Na Elinipa Lupembe
Uongozi wa halmashauri ya Arusha, umewapongeza walimu walioshinda tuzo ya Stadi za Ufundishaji kwa shule za Awali na Msingi nchini, tuzo
zilizotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania -TEA.
Katika mashindano hayo Mwl. Sophia Moses alikuwa mshindi wa kwanza na Mwl. Jenipher Chuwa akiwa mshindi wa pili wote wa shule ya Enaboishu Academy inayomilikiwa na Halmashauri ya Arusha, huku walimu 6 kati ya washindi 10 wa mwanzo wakitokea halmashauri ya Arusha.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu hao, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mhe. Dkt. Ojung'u Salekwa licha ya kuwapongeza walimu hao kwa ushindi, amekiri kuwa ushindi huo umeiletea sifa na heshima kubwa halmashauri yao kitaifa.
Ameweka wazi kuwa, ushindi huo unaweka wazi ushirikishwaji katika utumishi wa Umma, ukiimarishwa na usimamizi mzuri wa ufanyaji kazi kati ya walimu na halmshauri kupitia Idara ya Elimu Msingi.
"Nikuombe mkurugenzi, uendelee kutoa fursa kwa walimu za kujiendeleza kitaaluma pindi watakapohitaji kwenda masomoni, mwalimu anapokwenda masomoni licha ya kupata vyeti, inamuongezea ari ya kufanya kazi lakini zaidi umahiri wa stadi za kufundisha unaendana na mabadiliko ya kila siku ya kidunia" Amebainisha Mhe. Dkt. Ojung'u
Hata hivyo walimu hao licha ya kuishukuru serikali kwa programu hiyo ya kutoa tuzo kwa walimu, wameiponge
za programu ya mafunzo kazini MEWAKA, programu ambayo wamekiri kuwajengea uwezo wa kufundisha na kuwafanya kuwa mahiri katika stadi za ufundishaji.
Mwl. Jenipher Chuwa wa shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza Enaboishu Academy amesema kuwa program ya MEWAKA inawajengea uwezo wa kujiamini katika stadi za ufundishaji kwa kuwa walimu hukutana na kubadilisha uzoefu.
Afisa Elimu kata ya Oloirieni Mwl. Digna Swai, amesema kuwa walimu hukutana kwenye vituo vya walimu TRC na kujadilian a kwa pamoja mada tata, ambao hubadilisha uzoefu wa ufundishaji na matumizi ya zana rahisi za kufunfishia.
"Vituo vya TRC vina vifaa vya TEHAMA ambavyo vinaturahisishia pia ujifunzaji kwa kujisomea matini ya mada mbalimbali zilizopo kwenye mtandao, hivyo programu ya MMEWAKA imetupa niafasi ya kukaa pamoja na kujifunza mada tata zinazowasumbua walimu" Amefafanua Mwl Digna na Afisa Elimu kata
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.