• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

BAADA YA BWENI LA WASICHANA, TASAF YAWAKUMBUKA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI OLDONYOWAS.

Posted on: June 18th, 2022

Na. Elinipa Lupembe.

Katika kutekeleza mkakati wa kuboresha miundombinu ya shule, serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF,  imewakumbuka wavulana wa shule ya sekondari Oldonyowas, kwa kutoa fedha kwa ijali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mabweni mawili ya wavulana shule ya sekondari Oldonywas, halmashauri ya Arusha, baada ya kujenga mabweni mawili ya wasichana shuleni hapo.

Akizungumza wakati wa kukagua maendeleo ya  utekelezaji wa mradi huo, mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameweka wazi kuwa, kwa mara nyingine tena, serikali kupitia mfuko wa TASAF imetoa fedha, kiasi cha shilingi milioni 320, kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya kulala wanafunzi wavulana 160, shule ya sekondari Oldonyowas, hii ni baada ya awamu ya kwanza kujenga mabweni mengine mawili ya wasichana kwa shule hiyo.

Mkurugenzi Msumi amethibitisha umuhimu wa shule hiyo kuwa na mabweni kwa wanafunzi wa jinsi zote, ni kutokana na asili ya mazingira ya eneo hilo, watoto wengi wanaishi mbali na shule na kusababisha kitembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni, jambo ambalo linawaathiri kiafya, kisaikolojia na hata kitaaluma.

"Ninampongeza Rais wetu, Mama Samia kwa kusikia kilio cha watoto wake, watoto wa Oldonyowas, na kujenga mabweni ya wavulana pia, tunaamini uwepo wa mabweni utaongeza ari ya wanafunzi kupenda shule, kutapunguza watoto kuacha shule, kwa kuwa na mazingira tulivu ya  kujisomea, jambo ambalo litapandisha taaluma shuleni na kuongeza kiwango ya ufaulu kwa wanafunzi " Amefafanua Mkurugenzi Msumi

Naye Michael Ismail mwanafunzi wa kidato cha nne, licha ya kuishukuru serikali ya awamu ya sita, amefurahishwa na kitendo cha kujengwa mabweni ya wavulana shuleni hapo, ambapo awali kulikuwa na mabweni ya wasichana peke yao na kuongeza kuwa wanafunzi wengi hukosa muda wa kujisomea wawapo nyumbani, kutokana na uchovu wa kutembea umbali mrefu, huku wazazi wakiwapangia majukumu ya kazi za nyumbani mara watokapo shuleni.

"Watoto wengi wanaishi mbali na shule lakini wakifika nyumba watapewa kazi za kuchunga ama kukata majani ya mifungo, jambo ambalo linatukosesha muda wa kujisomea hasa tuwapo nyumbani, lakini tukiwa na mabweni itatusaidia kutumia muda mwingi kujisomea kwa pamoja na kuturahisishia kufanya kazi za shule kwa kujadiliana katika makundi 'group discussion'". amefafanua mwanafunzi Michael

Mradi huo wa ujenzi wa mabweni mawili ya wavulana shule ya sekondari Oldonyowas, unafanya kuwa na idadi ya miradi tisa tofauti iliyotekelezwa na TASAF katika shule hiyo, ikiwemo vyumba vya madarasa, mabweni mawili ya wasichana, jengo la utawala, matundu ya vyoo, nyumba za walimu.

ARUSHA DC 

KaziInaendelea✍✍✍✍

JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022


Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi (wa kwanza kushoto)akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa mabweni ya wavulana shule ya sekondari Oldonyowas, QS. Bibie Manzi ( wa kwanza kulia)


Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi akiwangoza wakuu wa Idara na vitengo kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mabweni ya wavulana shule ya sekondari Oldonyowas.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.