Na Elinipa Lupembe
Hatimaye Shule ya sekondari Bangata, imekamilisha ujenzi wa chumba kimoja cha darasa, mradi uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 20 fedha kutoka Serikali Kuu, ikiwa ni maandalizi ya kupokea wananfunzi wa kidato cha kwanza, watakaopangiwa kwa mwaka wa masomo utakaoanza Januari 2023.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkuu wa shule hiyo, Mwl. Grace Minja, ameweka wazi kuwa, shilingi milioni 20 zimetumika kujenga chumba cha madarasa, meza na viti 40.
Aidha Mwl. Grace , ameitaja siri ya kukamilisha mradi kwa haraka ni hali uhitaji wa madarasa hayo moja, ari ya kazi na kujituma lakini zaidi matumizi ya force akaunti yanayoruhusu ushirikishwaji wa jamii katika kutekeleza.
"Tunamshukuru sana mheshimiwa Rais, shule ilikuwa na uhitaji wa vyumba vinne vya madarasa, na serikali ikaleta fedha za idadi inayolingana na ya uhitaji, uwepo wa madarasa ya kutosha unarahisisha tendo la kujifunza na kufundisha kwa wanafunzi na walimu, mazingira bora huwafanya wanafunzi kupenda shule". Amesema Mkuu huyo wa shule
Shule ya sekondari Bangata ni miongoni mwa shule mwa ahule za kata zinazokuwa kwa kasi ikiwa na jumla ya wanafunzi 377, wasichana 220 na wavulana 157 .
ARUSHA DC
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.