BARAZA LA WAFANYAKAZI ARUSHA DC LAJADILI NA KUPITISHA BAJETI YA 2025/2026
Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Arusha limejadili na kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya shilingi bilioni 68.1 kwa mwaka wa fedha 2025/2026, katika kikao maalum kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo mkoani Arusha.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bw. Seleman H. Msumi, alieleza kuwa kila mfanyakazi ana jukumu la kutimiza wajibu wake kwa kushirikiana ili kufanikisha malengo ya maendeleo ya Halmashauri hiyo. Alisisitiza kuwa ushirikiano na utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia Bajeti iliyopitishwa ni hatua muhimu ya kufanikisha adhima ya Halmashauri.
“Ni jukumu letu kuhakikisha tunazingatia sheria, taratibu, na miongozo katika kutekeleza majukumu yetu. Kila mmoja wetu ahakikishe anatimiza wajibu wake kwa bidii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi,” alisema Bw. Msumi.
Awali, akiwasilisha rasimu ya Bajeti hiyo, Afisa Mipango na Uratibu wa Halmashauri, Bi. Anna Urio, alifafanua kuwa jumla ya shilingi bilioni 7.2 zinatarajiwa kutoka vyanzo vya mapato ya ndani, shilingi bilioni 48.4 zitatumika kwa mishahara ya watumishi, shilingi bilioni 2.9 kwa ruzuku ya uendeshaji, na shilingi bilioni 9.6 kwa miradi ya maendeleo, fedha zote zikitolewa na Serikali Kuu.
Bi. Urio aliongeza kuwa mapendekezo na maazimio ya kikao hicho yamechukuliwa kwa umakini mkubwa, na ofisi ya Mipango na Uratibu imeahidi kushirikiana na idara mbalimbali ili kuhakikisha utekelezaji wa bajeti hiyo unaleta maendeleo chanya ndani ya Halmashauri.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Dkt. Paschal Daniel Kangiria, aliipongeza timu ya uandaaji wa bajeti kwa umakini na weledi waliouonyesha. Aidha, alisifu hatua za Halmashauri hiyo katika kuhakikisha kuwa mapendekezo ya bajeti yamezingatia maslahi ya wafanyakazi na maendeleo ya jamii.
Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Arusha limejadili na kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya shilingi bilioni 68.1 kwa mwaka wa fedha 2025/2026, katika kikao maalum kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo mkoani Arusha.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bw. Seleman H. Msumi, alieleza kuwa kila mfanyakazi ana jukumu la kutimiza wajibu wake kwa kushirikiana ili kufanikisha malengo ya maendeleo ya Halmashauri hiyo. Alisisitiza kuwa ushirikiano na utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia Bajeti iliyopitishwa ni hatua muhimu ya kufanikisha adhima ya Halmashauri.
“Ni jukumu letu kuhakikisha tunazingatia sheria, taratibu, na miongozo katika kutekeleza majukumu yetu. Kila mmoja wetu ahakikishe anatimiza wajibu wake kwa bidii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi,” alisema Bw. Msumi.
Awali, akiwasilisha rasimu ya Bajeti hiyo, Afisa Mipango na Uratibu wa Halmashauri, Bi. Anna Urio, alifafanua kuwa jumla ya shilingi bilioni 7.2 zinatarajiwa kutoka vyanzo vya mapato ya ndani, shilingi bilioni 48.4 zitatumika kwa mishahara ya watumishi, shilingi bilioni 2.9 kwa ruzuku ya uendeshaji, na shilingi bilioni 9.6 kwa miradi ya maendeleo, fedha zote zikitolewa na Serikali Kuu.
Bi. Urio aliongeza kuwa mapendekezo na maazimio ya kikao hicho yamechukuliwa kwa umakini mkubwa, na ofisi ya Mipango na Uratibu imeahidi kushirikiana na idara mbalimbali ili kuhakikisha utekelezaji wa bajeti hiyo unaleta maendeleo chanya ndani ya Halmashauri.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Dkt. Paschal Daniel Kangiria, aliipongeza timu ya uandaaji wa bajeti kwa umakini na weledi waliouonyesha. Aidha, alisifu hatua za Halmashauri hiyo katika kuhakikisha kuwa mapendekezo ya bajeti yamezingatia maslahi ya wafanyakazi na maendeleo ya jamii.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.