Na. Elinipa Lupembe.
Wananchi, Halmashauri ya Arusha wameungana na watu wote duniani, kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani, huku Baraza La watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU) halmashauri hiyo, likiwa na mafanikio na matumini makubwa ya kimaisha, kupitia uwezeshwaji unaofanywa kwa ushirikiano mkubwa kati ya ASASI za kiraia na halmashauri ya Arusha.
Wakizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Balbal kata ya Oloirieni halmashauri ya Arusha, WAVIU hao wameweka wazi kuwa, kutokana na uwezeshaji kupitia mafunzo mbalimbali ya kiafya, kijamii na kiuchumi, wanayoyapata kupitia Baraza hilo la WAVIU, Baraza limeweza kuwafanya watu wanaoishi na VVU, kujikubali na kujiamini kwa kuacha kujinyanyapaa wenyewe, kuimarika kiafya kwa kutumia ARV kwa ufasaha, kujiinua kiuchumi kupitia shughuli za ujasiriamali zinazofanywa kupitia vikundi vya WAVIU.
Mweka Hazina wa Baraza la WAVIU halmashauri ya Arusha, Trifonia Mdendemi, amethibitisha kuwa kupitia konga lao la WAVIU, baraza limefanikiwa kuwaunganisha kwenye vikundi takribani waathirika 280 wa VVU, vikundi ambavyo vimejengewa uwezo wa kujikubali, kuacha kujinyanyapaa, kutumia dawa za ARV kwa ufasa na kuwa mabalozi wa kuibua na kuwatia moyo WAVIU ambao wamekata tamaa, jambo ambalo limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 kupitia malengo ya mwaka huu wa 2021.
"Mpaka sasa tuna jumla ya vikundi 25 vya wajasiriamali WAVIU 280 katika kata 5, wote wamepata mafunzo ya kuwawezesha kufanya biashara ndogo ndogo, zinazowaingizia kipato cha familia, na kuziwezesha familia kumudu kupata mahitaji muhimu ya familia, jambo lililorejesha amani na matumaini makubwa kwa WAVIU wengi, tofauti na zamani WAVIU wengi walikata tamaa kwa kutengwa na jamii inayowazunguka na kujiona wao na wakufa tuu" amefafanua Trifonia.
Naye Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Selemani Msumi, amewapongeza WAVIU hao na kuwatia moyo kuendelea kuishi kwa matumaini, huku wakijiamini mbele ya jamii na kufanya kazi zao za uzalishaji mali kwa bidii, kazi ambazo licha ya kuingiza kipato cha familia lakini pia ni msingi wa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Ameongeza kuwa, halmashauri itaendela kushirikiana na ASAS za kiraia, kuwaimarisha na kuwajengea uwezo WAVIU hao, pamoja na kuhamasisha jamii, kupambana na maambukizi mapya ya VVU mpaka kufikia asilimia 95 ifikapo 2030, kuondoa unyanyapaa ndani ya jamii, pamoja na kuhakikisha WAVIU hao wanapata dawa za kufubaza makali ya VVU kwa wakati na kwa usahihi, kupitia vituo vyote vya kutolea huduma za afya.
"Nimevutiwa sana na maonesho ya shughuli mbalimbalai za kupambana na UKIMWI kiseta, nendelee kuwatia moyo ndugu zangu, serikali yenu makini iko pamoja na ninyi, kwa kuwa mnazidi kuuthibitishia Umma, kwamba UKIMWI ni ugonjwa kama magonjwa mengine, ugonjwa ambao ukijikubali na ukizingatia masharti yanayolelekezwa na wahudumu wa afya, na ukatumia dawa kwa usahihi, unaweza kuishi maisha marefu na kutimiza ndoto zako, tofauti na dhana iliyojengeka hapo awali, kwamba ukipata maambukizi ya VVU wewe ni wa kufa tuu" amesisitiza mkurugenzi huyo.
Naye Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Arusha, Upendo Elisamehe, Lengo la maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, ni kitoa fursa ya kutathmini hali na kuhusu uthibiti UKIMWI ambayo husaidi katika kubaini changamoto, mafanikio na kuwa na mkakati katika kupambana na maambukizi ya VVU pamoja na UKIMWI katika jamii zetu.
"Maadhimisho haya yanafanyika ili kuikumbusha jamiii kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi ya mapya ya VVU na kuwakumbusha watu wenye maambukizi kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU kwa ufasaha bili kuacha, kubwa zaidi, jamii kuacha unyanyapaa kwa watu wenye amambukizi na kuwapa huduma stahiki kwa upendo" amesisitiza Mratibu huyo wa UKIMWI.Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani halmashauri ya Arusha 2021, yamefanyika kwa ushirikiano wa halmashauri hiyo na mashirika ya ACE Africa, CWCD, Kizazi Kipya, HIMD huku kauli mbiu ikisisistiza 'Zingatia Usawa, Tokomeza UKIMWI, Tokomeza magonjwa ya Mlipuko'.
ARUSHA DC
#KaziIendelee✍
Mweka Hazina wa Konga la WAVIU halmashauri ya Arusha, Trofina Mdendemi (wa pili kushoto) akimuonyesha na kumuelezea mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi ( aliyevaa skafu) shughuli zinazofanywa na vikundi vya wajasiriamali wanaoishi na Virusi vya UKIMWI.
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi akizungumza na hadhara wa wananchi, wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMIWI Duniani, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Balbal kata ya Oloirieni halmashauri ya Arusha.
Makamu Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, na Diwani wa kata ya Matevesi, Mheshimiwa Freddy Lukuma akizungumza na hadhara wa wananchi, wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMIWI Duniani, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Balbal kata ya Oloirieni halmashauri ya Arusha.
Konga la WAVIU halmashauri ya Arusha wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi, wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMIWI Duniani, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Balbal kata ya Oloirieni halmashauri ya Arusha.
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi akisiskiliza mawsilisho ya namna ukeketaji unafanyika, kutoka kwa wadau wa shirika la HMD, maonesho yaliyofanyika wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMIWI Duniani, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Balbal kata ya Oloirieni halmashauri ya Arusha.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.