• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

BILIONI 3.3 ZATEKELEZA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA ROBO YA KWANZA JULAI - SEPTEMBA, 2022

Posted on: October 31st, 2022

Na Elinipa Lupembe 

Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji na utoaji wa huduma kwa wananchi, kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo katika halmashauri nchini, huku Halmashauri ya Arusha, ikiwa miongoni mwa halmashauri iliyonufaika kwa kupata fedha kiasi cha shilingi bilioni 3. 27 kutoka Serikali Kuu ikiwa ni fedha za  utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 ukioanza Julai 1, 2022.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amethibitisha kuwa shilingi bilioni 3.3 zinatumika kutekeleza shughuli za mbalimbali za halmasahuri hiyo ikiwemo utekelazaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya kuanzia Julai - Septemba kwa mwaka wa fedha 2022/2023.


Msumi ametaja fedha hizo ni kuwa,  kiasi cha shilingi bilioni 3.27 ni kutoka fedha kutoka Serikali Kuu na shilingi milioni 95.2 zikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya halmashauri, na utekelezaji wake unaendelea kukamilika.

Aidha ameutaja mchanganuo wa fedha hizo kuwa milioni 658.4 fedha za elimu bila malipo wa idara ya  msingi na sekondari huku milioni 227.9 elimu msingi na milioni 430 kwa elimu sekondari na kuongeza kuwa shilingi  milioni 589.5 zikitumika katika utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya shule pamoja na  milioni 187.8 fedha za kuendesha shughuli za mitihani ya Taifa.

Katika sekta ya Afya serikali imetoa shilingi milioni 502.6, kwa mchanganuo wa milioni 52 kwa ajili ya shughuli za chanjo, milioni 50.6 fedha za Mpango wa Kudhibiti UKIMWI, milioni 50 ujenzi na ukamilishaji wa zahanati ya Mirongoine pamoja na milioni 350 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

Hata hivyo serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) halmashauri imepokea kiasi cha shilingi 602, fedha kwa ajili ya walengwa 13, 920 walio kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini.

Aidha mkurugenzi Msumi amefafanunua kuwa serikali imetoa shilingi milioni 760 nje ya bajeti kwa jaili ya ujenzi wa vyumba 38 vya madarasa kwa shule 15 za sekondari ikiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidaato cha kwanza wanaotegemea kupangiwa kwenye shule za serikali kwa mwaka wa masomo 2023.

"Fedha zote hizo tayari zimetekelezwa kulingana na shughuli zilizopangiwa, huku utekelezaji wa miradi ya maendeleo ukitumia 'Force' Akaunti kwa kutumia mafundi wazawa chini ya usimamizi wa kamati za ujenzi zinazoundwa kisheria na wananchi wa maeneo husika" Amesisitiza Mkurugenzi Msumi


ARUSHA DC

KaziInaendleea ✍✍



MGAWANYO WA FEDHA NI KAMA UNAVYOONEKANA KWENYE JEDWALI MDUARA


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.