Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Emanuela Kaganda, amewataka wakazi wa halmashauri ya Arusha, kuuenzi, kuulinda na kuutetea Muungano kwa kushirikiana kufanya kazi kwa bidii juhudi na maarifa ili kuendelea kutunza na kuimarisha tunu za Muungano.
Mhe. Emmanuel, ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano, uzinduzi uliofanyika kwenye shule ya sekondari Mringa kata ya Oloirieni, halmashauri ya Arusha.
"Leo tunazindua rasmi wiki ya Maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano tangu nchi za Tanganyika na Zanzibar kuungana, Muungano ambao umebebwa na misingi ya Uhuru na Umoja, tunapaswa kufahamu kuwa misingi hiyo ndiyo nguzo ya Taifa letu la Tanzania na wananchi wa pande zote mbili". Amefafanua Mkuu huyo wa wilaya.
Mh. Emmanuela amewasisitiza wananchi wa Wilaya ya Arumeru kuutetea, kuupigania, kuusimamia na kuulinda Muunga kwa nguvu zote, sambamba na kutoa elimu sahihi kwa wananchi wengine ambao hawana taarifa sahihi kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
"Ndugu zangu tusimame kkidete, tusimame imara kuutetea, kuupigania, kuusimamia na kutoa elimu sahihi kwa wananchi wengine ambao hawaufahamu vizuri Mmuungan, tuwafundishe watoto wetu kuhusu Muungano na tunu zake, someni na shirikini kwenye midahalo inasaidia kupata maarifa na kkutjenga kupitia taarifa mbalimbali zinazotolewa kwenye vyombo vya habari kwa manufaa ya nchi yetu". Amesisitiza Mkuu huyo wa wilaya.
Aidha amewapongeza waasisi wa Muungano Hayati Mzee Abeid Karume na Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa maamuzi yayaya busara na muhimu kwa watanzania kwa kuunganisha nguvu, kwa kuwa Umoja ni nguvu na uengano ni udhaifu.
Amezitaja Sababu za msingi za kuungana Tanganyika na Zanzibar, ni ukaribu wa nchi hizi mbili uliosababisha muingiliano wa kijamii, udugu wa damu kati ya wananchi nchi hizi mbili, pamoja na mwingiliano wa kibiashara pamoja na urafiki, undugu na uongozi wa pande zote mbili.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa Muungano huu, umeongeza wigo kwa wananchi wa pande zote mbili kuendelea kutumia kutumia fursa zinazopatikana kati ya Tanzania Bara na Visiwani, fursa amamba licha ya kudumisha udugu, zina lengo la kuleta maendeleo kwa watanzania wa pande zote.
"Tunayashuhudia, matunda ya Muungano yanayoyojengwa kwenye misingi ya uhuru na umoja, iliyobeba dhana kubwa ya upendo, amani na mshikamano wenye dhana ya udugu wa enzi na enzi, niwatake ndugu zangu, kila mmoja kusimamia misingi ya Muungano kwa kuutunza, kuulinda na kuenzi mambo yote mema kwa manufaa ya watanzania wote kwa ujumla wake". Amefafanua Mkuu huyo wa wilaya
Kauli mbiu ya Muungano 2023: "Umoja na mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu"
PPCHA ZA MATUKIO
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.