• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC Arumeru awafunda Maafisa Tarafa, Maafisa Watendaji Kata na Vijiji

Posted on: February 1st, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro, amewataka Maafisa watendaji wa kata na vijiji wilayani humo, kufanya kazi kwa bidii  kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, kwa kuweka mbele maslahi ya taifa ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa rai hiyo, wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha maafisa tarafa na Maafisa watendaji wa kata na vijiji wa halmashauri zote mbili za wilaya ya Arumeru, chenye lengo la kuwakumbusha na kuwajengea uwezo watalamu hao katika kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

Amesema, kama wilaya wamemekubaliana kuanzisha programu maalumu ya mafunzo kwa watendaji hao, kwa kushirikiana na chuo kilichopo ndani ya wilaya hiyo, chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, baada ya kugundua uhitaji wa mafunzo kwa watalamu hao, mafunzo yatakayowawezesha kuwa na uelewa wa pamoja katika kuteleleza majukumu yao.

Amesema kuwa Maafisa hao huajiriwa kutoka kwenye kada tofauti, jambo ambalo wakati mwingine, linalopelekea changamoto ya kukwamisha baadhi ya kazi, kupitia mafunzo hayo yatawawezesha kuwa na uelewa wa pamoja na kufahamu majukumu yao na mipaka ya kazi yao, kufanya kazi kwa uadilifu, kujiamini, kuongeza ari na morari ya kazi, pamoja na kuweka mbele uzalendo kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

"Tumegundua kuna umuhimu kupata mafunzo kwa watendaji wote, yatakayowakumbusha na kuwawezesha kutambua namna sahihi ya utekelezaji wa kazi zenu za kila siku, hii imetokana na baadhi ya watendaji kushindwa kutekeleza majukumu yenu kwa usahihi na kusababisha malalamiko mengi kwa wananchi" amesema Mkuu huyo wa wilaya.8

Hata hivyo Mhe. Muro amewasisitiza watendaji hao kusimamia hali ya  usalama katika maeneo yao, kwa kutambua wageni wanaoingia na kutoka katika maeneo yao, kuhamasisha wananchi kushiriki kuchangia maendeleo katika maeneo yao, huku kipaombele kikiwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa hususani kwenye shule za sekondari, lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serekali la kutoa  elimu bila maliopo linalotoa fursa ya kila mtoto kupata nafasi ya kusoma mpaka kidato cha nne.

"Kazi kubwa ya mwaka huu ni kujenga vyumba vya madarasa, ninawaomba Maafisa Watendaji, tuelekeze nguvu zetu kuhamasisha jamii kujikita katika kujenga madarasa, nataka nione kila Tarafa ina shule ya kidato cha 5-6 na kila kata ya kidato cha 1-4" amesema Mhe. Muro

Kwa upande wao wakurugenzi wa halmashauri zote mbili, wamewataka Maafisa Watendaji hao kusimamia shughuli za maendeleo kwa kuendana na kasi ya serikali iliyopo madarakani,serikali ya awamu ya tano, kuwa waadilifu katika  kutekeleza kazi zao, kutoa huduma sawa kwa wananchi na kusimamia haki, na kuongeza kuwa hawatosita kuwachukulia hatua wale wote watakaofanya kazi kinyume na maadili.

Kikao kazi hicho, kiliambatana na mafunzo yaliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii kutoka chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Mkufunzi Douglas Mwadolago, mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo watendaji hao ya mbinu bora  za kuhamasisha jamii, kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Hata hivyo watendaji  hao, wamesifu juhudi zinazofanywa na halmashauri zao kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya, na kusema kuwa mafunzo hayo yanawaongezea ujuzi na maarifa zaidi ya kutekeleza kazi zao na kuahidi kwenda kutumia maarifa waliyoyapata katika kazi zao za kila siku.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kikuletwa kata ya Mbuguni, halmashauri ya Meru, Flora Maghimbi amesema kuwa, amefurahishwa na mafunzo hayo na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi, huku akiahidi pia kutekeleza maagizo yaliyotolewa kwa kuwa yote yanalenga maslahi ya jamii wanayoihudumia.

Awali, Wilaya ya Arumeru inaundwa na halmashauri mbili, halmashauri ya Arusha na Meru, ikiwa na jumla ya Tarafa  6, kata 53 na vijiji193


*PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KIKAO KAZI HICHO* 

Baadhi ya Maafisa Watendaji wa kata wakifuatilia maagizo ya mkuu wa wilaya ya Arumeru, walipokutana na kwenye kikao kazi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

                         -------------------------------------------------------------------

Katibu Tawala wilaya ya Arumeru, Mwalimu James Mchembe, akizungumza na Maafisa Watendaji wa kata na vijiji, wakati wa kikao kazi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha

                 ---------------------------------------'---------------------------------

Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera, akizungumza na Maafisa Watendaji wa kata na vijiji, wakati wa kikao kazi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

                  -------------------------------------------------------------------------

Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Meru Emanuel Mkongo, akizungumza na Maafisa Watendaji wa kata na vijiji,  wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.

                   --------------------------------------------'---------------------




Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MKATABA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA August 14, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KUFUATILIA NA USAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KATIKA JAMII NI JAMBO MUHIMU

    August 25, 2025
  • RAIS SAMIA AMUAPISHA AMOS MAKALLA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    August 26, 2025
  • DKT. JAHANNES LEMBULUNG' LUKUMAY ACHUKUWA FOMU YA UGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI

    August 25, 2025
  • KIKAO KAZI CHA WENYEVYITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA (CEOs Forum 2025)

    August 24, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.