• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC ARUMERU AWATAKA WALIMU KUONGEZA BIDII KWENYE KAZI 2023.

Posted on: January 7th, 2023

Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, amewataka walimu  kuanza mwaka wa masomo 2023, kwa  kuongeza bidii na maarifa zaidi katika kufanya kazi ili kuhakikisha wanafunzi wanafundishwa na hatimaye kufanya vizuri kwenye masomo yao kama ilivyokuwa mwaka uliopita wa 2022.

Mheshimwa Ruyango amesema hayo wakati akitoa salamu za mwaka mpya alipokutana na watalamu wa idara za elimu msingi na sekondari, halmashauri ya Arusha wakiwemo wakuu wa shule za sekondari,  walimu wakuu wa shule za msingi pamoja na Maafisa Elimu kata, kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya licha ya kuwapongeza walimu kwa kufanya kazi nzuri mwaka 2022, kazi ambayo tayari matokeo ya mitihani ya kitaifa yametoa tathmini ya utumishi ulio bora kwa walimu, wanafunzi, wazazi na wadau wa elimu wilaya ya Arumeru.

"Ninatambua kazi kubwa mliyoifanya walimu mwaka 2022, tumepambana kwa umoja wetu, kuhakikisha wanafunzi wamefundishwa na kuweza kufanya vizuri mitihani yao ya ndani na ile ya Taifa na kumaliza mwaka salama, ninawapongeza sana na niwatake mwaka 2023 kwa pamoja tuongeze bidii zaidi". Ameweka wazi Mkuu huyo wa wilaya.

Amesisitiza kuwa, walimu wana dhamana kubwa ya maisha ya watu, kwa kuwa mwalimu ndio kiwanda cha kuzalisha watalamu wote duniani, na kuwataka kutumia dhamana hiyo kuzalisha watalamu ambao ndio wajenzi wa Taifa hili.

"Shule zinafunguliwa Jumatatu ya tarehe 09, Januari 2023, hakikisheni wanafunzi wote wanaotakiwa kuwa shuleni wamefika na kuanza masomo mara moja, wanafunzi waliopangiwa kuajiunga na kidato cha kwanza walimu hakikisheni wameripoti shuleni kwa idadi yao, kama kuna changamoto yoyote toeni taarifa ili iweze kupatiwa ufumbuzi mapema". Amesema Mhandisi Ruyango

Aidha ameutaka uongozi wa halmashauri licha ya kusimamia ufanyaji kazi wa watumishi, usimamizi huo uende sambamaba na kusimamia maslahi ya watumishi kwa kuhakikisha kila mtumishi anapata haki zake za kisheria kama miongozo ya utumishi inavyoelekeza,  jambo litakalomfanya mtumishi kuwa na moyo wa kutekeleza majumu yake.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amekiri kupokea maelekezo hayo na kuyafanyia kazi kulingana na taratibu za Utumishi wa Umna na kuongeza kuwa halmashauri inatambua na kuthamini kazi kubwa ya kuwahudumia wananchi inayofanywa na watumishi wa kada zote.

Hata hivyo walimu wamemshukuru na kumpongeza mkuu huyo wa wilaya, kwa kukutana na walimu na kuahidi kushirikiana kwa pamoja kufanya kazi kwa bidii zaidi na kuhakikisha wanafunzi wanapata ujuzi na maarifa utakao wawezesha kupandisha kiwango cha taaluma.

Aidha wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongzwa na mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia shuleni ikiwe miundombinu ya madarasa, nyumba za walimu pamoja na vifaa vya kiditali vya kufundishia.


ARSHA DC

KaziInaendelea✍✍

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango akitoa salamu za Mwaka mpya kwa watalamu wa elimu msingi na sekondari wakiwemo wakuu wa shule za sekondari, Maafisa Elimu ngazi ya kata na halmashauri, Walimu Wakuu shule za masingi halmashauri ya Arusha, kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha akizungumza kwenye mkutano uliojumuisha  watalamu wa elimu msingi na sekondari wakiwemo wakuu wa shule za sekondari, Maafisa Elimu ngazi ya kata na halmashauri, Walimu Wakuu shule za masingi halmashauri ya Arusha, kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari,  walimu wa  wakuu shule za msingi na Maafisa Elimu kata wakiwa kwenye mkutano na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango,  kwenye ukumbi wa  mkutano halmashauri ya Arusha 

Walimu wakuu wa shule za sekondari,  walimu wakuu shule za msingi na Maafisa Elimu kata wakiwa kwenye mkutano na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango,  kwenye ukumbi wa  mkutano halmashauri ya Arusha 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.