Kuelekea sherehe za maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Emmanuela Kaganda, amezindua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madara, shule ya sekondari Mringa, halmashauri ya Arusha.
Akizingumza wakati wa kuzindua mradi huo, amewapongeza wananchi, viongoz na watalamu wa halmashauri ya Arusha, kwa usimamizi imara wa miradi, hali inayothibitisha uzalendo kwa taifa la Tanzania.
Akisoma taarifa ya mradi huo, mkuu wa shule ya sekondari mringa Mwl. Salum Magaka, amesema kuwa shule hiyo ilipokea shilingi milioni 80 na zimetumika kujenga vymba vinne vya madarasa, viti na meza 200, madaras amabayo yalikiwa ni maalumu kwa kuwapokewa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.
Amefafanua kuwa, kukamilika kwa vyumba hivyo vya madarasa, umewezesha kupokea jumla ya wanafunzi 576 kati ya hao wasichana ni 342 na wavulana 234 kati ya wanafunzi 728 waliopangiwa shuleni hapo.
Kauli mbiu ya Muungano 2023: "Umoja na mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.