• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC ARUMERU Mhe. EMMANUELA MTATIFIKOLO AMEFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA NGO's ARUSHA DC..

Posted on: May 22nd, 2023

Na Elinipa Lupembe


Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, amefungua mkutano wa tathmini wa mwaka wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kwa mwaka 2022, halmashauri ya Arusha, mkutano unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.


Akifungua mkutano huo, Mhe. Emmanuela licha ya kutambua, kushukuru na kuthamini kazi zinazofanywa na mashirika hayo, ameyataka mashirika hayo kufanyakazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na miongozo ya nchi hasa kwa kutekeleza miradi inayozingatia vipaumbele vya maendeleo vya Taifa pamoja na kuzingatia maadili, mila na desturi za kiTanzanzia.


"Tunataka mashirika kutekeleza miradi inayotoa hudma za jamii na kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa, na si vinginevyo, tunatambua changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wetu lakini miradi hiyo izingatie vigezo vya Taifa na maendeleo ya jamii husika". Amefafanua Mhe. Emmanuela.


Aidha ameyataka mashirika hayo kufanya kazi kwa uwazi kwa kushirikiana na watalamu na  viongozi wa ngazi zote kuanzia ngazi ya wilaya, halmashauri, kata, vijiji na vitongoji pamoja na kuwashirikisha wananchi wa maeneo ambayo miradi inayotekelezwa.


Zaidi Mkuu wa wilaya huyo ameyasisitiza mashirika hayo kufanya kazi kwa uwazi kwa kuitambulisha miradi hiyo na kuhakikisha wananchi wanaifahamu vizuri miradi inayotekelezwa katika maeneo yao, gharama za mradi, muda wa utekelezaji pamoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi hiyo kila robo ya mwaka kwa idara husika.


"Hatutasita kuyachukulia hatua za kisheria mashirika yote yasiofuata taratibu za serikali, yapo mashirika yasiyowasilisha taarifa kulingana na taratibu na maelekezo ya serikali kwa kila robo, mashirika hayo tutayashughulikia kwa mujibu wa sheria, Niyatake mashirika yote kufuata taratibu". Amefafanua Mkuu huyo wa Wilaya.


Mkutano huo  wa mwaka ni wa kisheria unalenga kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO's) kuanzia Januari - Desemba 2022, wenye lengo la kufanya tathmini ya miradi ya iliyotekelezwa kwa mwaka.


ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.