• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC Jerry Muro akutana na watumishi wa Arusha DC

Posted on: August 1st, 2018

Na. Elinipa Lupembe.

Mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro leo amepata fursa, ya kukutana na kuzungumza na watumishi wa halmashauri  ya Arusha kwa mara ya kwanza, moja kati ya halmashauri mbili za wilaya hiyo ya arumeru, mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.  

Mkuu huyo wa wilaya, amekutana na watumishi wa halmashauri hiyo, wakati akitambulishwa kwao, na mkuu wa wilaya ya Monduli mheshimiwa Idd Kimanta,  aliyekuwa akikaimu ukuu wa wilaya ya Arumeru, kwa takribani miezi nane sasa.

Mheshimiwa Muro baada ya kutambulishwa, amewataka watumishi wa halmashauri ya Arusha, kufanyakazi kwa bidii na uadili  mkubwa, huku wakifuata kanuni na madili ya kazi na kuwasisitiza kuwa wanyenyekevu na wakarimu katika kuwahudumia wananchi.

Ameongeza kuwa, anafahamu mheshimiwa Rais John Pombe Mgufuli,  anahitaji kuwahudumia wananchi wanyonge,  hivyo watumishi wote wa serikali ni lazima watoe huduma bora kwa kuwajali sana wananchi na si kutoa huduma kwa ubabaishaji.

"Ninachowaka watumishi wa Arusha DC, tucheze ngoma ya pamoja,  ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ngoma yenye lengo la kuwahudumia wananchi walio wanyonge, kwa kuwajali wananchi wote, kama yalivyo matakwa ya mheshimiwa Rais wetu"  amesema mkuu huyo wa wilaya

Aidha amewaonya,  wale wanaodhani kuwa kasi  ya rais Magufuli, ni nguvu ya soda wanajidanganya, huku akifafanua kuwa anachokitamka na anachofanya, mheshimiwa Rais, anamaanisha na hana utani na watumishi waonaokwenda kinyume na taratibu za nchi hii.

"Narudia kusema tena na tena, jamanii asiyetaka kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, atupishe, na ikiwezekana tupishane mapema pale tuu, ninapoingia ofisini" amesisitiza mkuu huyo wa wilaya 

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa watumishi hao, mheshimiwa Muro amemuagiza Afisa Maendeleo ya Jamii, halmashauri ya Arusha, kuandaa andiko la kuanzisha SACCOS ya wafanyakazi, ili kuwawezasha watumishi hao, kuweka na kukopa.

Ameahidi kuhakikisha SACCOS hiyo inasimamiwa vizuri, huku akisisitiza kuwa hawezi kufanyakazi na watumishi wasio na fedha na wenye njaa kali, jambo linalowasababisha kupokea rushwa na kufanya ubadhilivu kwenye fedha za Umma.

Mtumishi mwenye njaa, ni rahisi kushawishika, kuomba na kupokea rushwa pamoja na kutamani fedha za miradi na kuwasisitiza watumishi hao, kujipanga kuanzisha SACCOS,  itakayowezesha wafanyakazi wote kujiinua kiuchumi.

Naye mkuu wa wilaya ya Monduli,  baada ya kumtambulisha mkuu huyo mpya wa wilaya ya Arumeru, alitamka kumkabidhi watumishi wa Arusha DC wakiwa weupe, wenye afya njema, wanyenyekevu na wachapakazi na kuwataka watumishi hao, kumpa ushirikiano mkuu huyo wa wilaya kama ilivyokuwa kwake, kwa kipindi kifupi alichofanya katika halmashauri ya Arusha.  

Nao Watumishi wa halmashauri ya Arusha, wamempongeza mkuu wa wilaya ya Arumeru kwa kuaminiwa na kuteluliwa kwake,  na kuahidi kushirikiana nae kufanyakazi kwa weledi kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi,  kwa kasi ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tuu.

Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru mheshimiwa Jerry Muro, ameanza kazi rasmi leo ya kuwatumikia wanaArumeru, mara baada ya kuapishwa jana na mkuu wa mkoa wa Arusha, mheshimiwa Mrisho Gambo mara baada ya kuteuliwa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mwishoni mwa wiki iliyopita.

Matangazo

  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA TATU 2O21/2022 tarehe 09.05.2022 May 08, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA ARUSHA DC,BW.SELEMAN MSUMI AKIWA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO KATIKA MASDHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA ARUSHA

    May 02, 2025
  • HERI YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • HERI YA SIKU YA MEI MOSI

    May 01, 2025
  • MHE. MAJALIWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.