DC KAGANDA AKUTANA NA AFANYA KIKAO NA WADAU WA TAASISI ZA FEDHA
Mkuu wa wilaya ya Arumeru leo Julai 18, 2024 amekutana na kufanya kikao na wadau wa Taasisi za Kifedha ikiwa ni maandalizi ya kongamano la vijana na wanawake litakalofanyika Wilaya ya Arumeru hivi karibuni.
Katika kikao hicho Mhe. Kaganda amewaomba wadau hao kushiriki katika kutoa mafunzo ya fursa za mikopo mbalimbali kwa Wanawake, Vijana na Makundi maalum ikiwa ni adhma yake ya kuendelea kuinua uchumi wa Wananchi wa Wilaya ya Arumeru.
"Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametuonyesha njia kutokana na kasi ya maendeleo nchini, hivyo ni jukumu letu sisi wasaidizi wake kuyabeba na kutembea na maono yake kwa kuhakikisha tunawaunganisha Wananchi na Taasisi za Kifedha ili kuweza kupata fursa za kupata mikopo ya riba nafuu ikiwemo ile ya Serikali ya asilimia 10%. Alisema Kaganda
Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Benki ya CRDB pamoja na NMB huku wakiahidi ushiriki mzuri katika yale waliyojadili kwenye kikao hicho
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.