Na Elinipa Lupembe
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amefungua rasmi mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa shule za msingi - UMITASHUMTA ngazi ya wilaya, yanayofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Ilboru.
Akizungumza na wanamichezo hao, amewataka kufanya juhudi kwenye michezo hiyo muhimu kwa halmashauri, ili wapate nafasi ya kuchaguliwa, na kuunda timu zitakazoshiriki UMITASHUMTA ngazi ya mkoa.
"Niwaombe sana wanamichezo wote kuwa na munkari ya ushindi, pale mtakapoingia viwanjani, kujituma ili kuchaguliwa, kwenda kuiwakilisha halmashauri yetu, ngazi ya mkoa, kwa kuwa na nidhamu kusikiliza maelezo ya makocha, pamoja na kufuata kanuni na sheria za mchezo". Amesema Msumi
Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi, Mwl. Alute Salvatory, amesema kuwa, wanamichezo hawa ni washindi kutoka klasta tano za Mateves, Mlangarini, Sekei, Mringa, Ngaramtoni na Oldonyosambu, ambao wanategemewa kuchujwa na kupata timu itakayotuwakilisha UMITASHUMTA ngazi ya mkoa.
Naye mratibu wa michezo ya UMITASHUMTA halmashauri ya Arusha, Mwl. Khalifa Kiembe, amesema kuwa, wanamichezo hao wameandaliwa vizuri, kimwili na kisaikolojia kupitia walimu wao shuleni, wako hapa wakiwa na matumaini ya kwenda kuleta ushindi kama ilivyokuwa Mwaka 2022.
"Watoto hawa wana vipaji na wanamwamko mkubwa na hamasa ya michezo, walizopata kupitia wachezaji wa timu kubwa za ndani na nje ya nchi, hivyo kazi yetu walimu ni maelekezo tu, kwa kuwa tayari wanoa mwamko wa ndani" Amefafanua Mwl. Kiembe
Afisa Michezo Halmashauri ya Arusha, Mwl. Priscus Silayo, amesema kuwa amesema kuwa mashindano hayo yalianzia ngazi ya shule, kata, klasta na hatimaye tunaanza ngazi ya wilaya kwa kufuata muongozo wa ofisi ya Rais - TAMISEMI wa mwaka 2023
Amesema kuwa mashindano hayo yamejumuisha wanamichezo 400 kutoka klasta tano za halmashauri na wanategemewa kuwachujwa na kupata wanamichezo ya 120 watakao kwenda kushiriki UMITASHUMTA ngazi ya mkoa.
"Mashindano haya yanajumuisha michezo ya soka, mpira wa netiboli, wavu, kikapu, mikono riadha mpira wa goli, riadha maalum na kikapu ambayo ni michezo mipya katika mashindano ya UMITASHUMTA 2023.
Kaulimbiu ya UMISEMTA 2023: "Uimarishaji wa miundombinu nchini ni chachu ya Maendeleo ya Taaluma, Sanaa na Michezo nnchini
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.