Na Elinipa Lupembe
Mkurugezenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi mapema leo amekabidhiwa Vishikwambi 1, 422 vilivyotumika kwenye Sensa ya Watu na Makazi 2022.
Mkurugenzi Msumi amekabidhiwa Vishikwambi hivy na Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule, halmashauri ya Arusha, Fatuma Lema, kwa ajili ya kuwagawia watalamu wa elimu ikiwemo Maafisa elimu ngazi ya halmashauri na kata pamoja na walimu wa shule za msingi na msingi.
Fatuma ameweka wazi kuwa, halmasahuri ya Arusha imepokea jumla ya vishikwambi 1, 422, na kuvikabidhi kwa mkurugenzi tayari kwa kuvigawa kwa watalamu wa elimu.
Ikumbukwe kuwa, serikali ilitoa tamko kuwa vishikwambi vilivyotumika kwenye Sensa ya Watu na Makazi kugawiwa walimu nchini lengo likiwa kuimarisha somo la TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.
ARUSHA DC
KaziIendelee✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.