Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya sekondari Oljoro kata ya Laroi, mradi unaotekelezwa unaogharimu shilingi milioni 40 fedha kutoka serikali Kuu, ikiwa ni maandalizi ya mapekezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza Januari 2023.
Mkuu wa shule sekondari Oljoro Mwl.Doita Mwanyika, amebainisha kuwa kiasi hicho cha fedha kimetumika kujenga vyumba 2 vya madarasa, ofisi ya walimu yenye viti na meza 2, pamoja na viti na meza 40 vya wanafunzi.
Ujenzi umefikia asilimia 90 na unategemea kukamilia kabla ya tarehe 05 Desemba 2022.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.