Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua nyumba ya mtumishi wa afya zahanati ya Nameloki kijiji cha Losinoni juu kata ya Oldonyowas.
Ujenzi wa nyu,ba hiyo ya mtumishi umegharimu takribani shilingi milioni 30, Mradi umetekeleza na wanachi wa kijiji cha Losinoni Juu kwa ufadhili wa marafiki kutoka nchini ujerumani.
Akizungumza kwa niaba ya wafadhili hao, raia wa ujerumani, Andreas Reinke, amesema kuwa wamefikia uamuzi huo, mara baada ya kuona adha wanayoipata wakazi wa Losinoni Juu kwa kukosa huduma za afya kwa wakati.
Amebainisha kuwa mwaka 2018 marafiki wa Losinoni waishio Ujerumani, walijenga zahanati hiyo ya Nameloki na kuona bado kuna tatizo la mahali pa kuishi daktari, mwaka huu 2022, wamefanikisha ujenzi nyumba ya daktari.
"Tumejenga nyumba ya mtumishi ili kuwahakikishia wananchi wa Nameloki wanapata huduma za afya kwa muda wote, ni furaha yetu kuona watu wanapata huduma za kiamii katika maeneo yao". Ameweka wazi Andreas.
Aidha nyumba hiyo imejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 30, kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wanachi wa kijiji hicho kwa muda wote.
Hata hivyo baada ya ujenzi wa Zahanati hiyo, kwa mwaka wa fedha 2022/2023, tayrai serikali imeajiri watumishi watatu, wa kufanyakazi katika zahanati hiyo, pamoja na kutoa vifaa tiba ili wanachi wa eneo hilo wapate huduma za afya na kuondoa vifo vya kina mama na watoto.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha,Seleman Msumi, licha ya kuwashukuru wafadhili hao kwa kuunga mkono na kutekeleza vipaumbele vya Taifa, amewaahidi kuendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto za kijamii zinazowakabili wananchi wa Losinoni Juu.
Aidha Mkurugenzi Msumi amewataka wananchi wa Losinoni Juu, kuutunza mradi huo pamoja na wahudumu wa afya waliopangiwa kufanya kazi hapo, ili udumu kwa sasa na vizazi vijavyo.
"Wananchi wa Losinoni Juu, mmepata zahanati, serikali imeleta madaktari hapa, hakikisheni mnatunza miundo mbinu na mali zote pamoja na kushirikiana na watumishi hawa, ni ndugu zenu, ni watanzania wenzetu". Amesistiza Mkurugenzi Msumi.
ARUSHA DC
#KaziIendelee✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.