Na Elinipa Lupembe
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amewataka mafundi waliopewa kandarasi za ujenzi wa miradi inayoendelea kwenye halmashauri hiyo, kuongeza kasi ya kufanya kazi, ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati kulingana na mikataba yao.
Mkurugenzi Msumi ameyasema hayo, wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya elimu na afya inayotekelezwa katika halmashauri hiyo na kukutana na mafundi wakiendelea na kazi za ujenzi.
Aidha amewasihi wakandarasi hao, kutambua kuwa miradi ya serikali ina muda wake maalum wa utekelezaji kulingana na malengo ya mradi, na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha kazi hizo kwa wakati.
"Serikali imewaamini na kuwapa dhamana ya kufanya kazi hizo, wapo walioomba wakakosa, tumieni fursa hii mliyopewa kufanya kazi zenye ubora pamoja na kukamilisha kwa wakati ulio kwenye mikataba yenu, kinyume na hapo mtapoteza sifa na kuvunjiwa mikataba yenu". Amesisitiza Msumi
Hata hivyo Mkurugenzi amezitaka kamati za usimamizi wa miradi hiyo ngazi ya jamii, kuwabana wakandarasi hao na kuhakikisha mafundi wanakuwa kazini 'site' wakati wote.
Akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Zahanati ya Mirongoine, amewasitiza kuwabana mafundi waliowapa kazi kwa kuhakikisha wanafuata ratiba yao ya kazi waliyoiwasilisha kwenye mkataba, kwa kufanya hivyo ujenzi utakamilika kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi, Zahanati ya Mirongoine, Ibrahimu Lemeirudi licha ya kuishukuru serikali kwa kuwapa fedha milioni 50 za kukamilisha ujenzi wa zahanati yao, ameipongeza serikali kwa kutumia force akaunti, utaratibu unaowapa fursa wananchi kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa utaratibu huu, unawapa fursa wananchi kuilinda miradi hii na kufahamu hatua zote za utekeleza na kuhakikisha hakuna ubadhilifu wala upotevu wa fedha na mali ya Umma.
"Serikali kutumia kamati za wananchi, inasaidia usimamizi wa karibu, tunafahamu hatua zote za mradi, kuanzi mikataba, manunuzi, mapokezi ya vifaa na utunzaji, matumizi ya fedha zote za ujenzi hadi kulipia huduma zote kwa usimamizi wa watalamu wa halmashauri,lakini zaidi wananchi tunatambua mradi huu ni mali yetu". Amebainisha Mwenyekiti wa kamati.
Awali mkurugenzi huyo akiambatana na timu ya menejimenti (CMT), wamekagua miradi yenye thamani ya shilingi milioni 470, inayoendelea katika kata Laroi, Oljoro, Bwawani, Nduruma na Mlangarini.
ARUSHA DC
KaziInaendelea✍✍
MATUKIO YA UKAGUZI WA MIRADI KATIKA PICHA
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akizungumza na mafundi wanaojenga maabara ya shule mpya ya sekondari Olomitu kata ya Mlangarini, wakati akikagua utekelzaji wa miradi inayoendelea kutekelzwa katika halmasahuri hiyo
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi zahanati ya Mirongoine kata ya Oljoro Bw. Ibrahim Lemeirudi, wakati akikagua utekelzaji wa miradi inayoendelea kutekelzwa katika halmasahuri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akikagua ujenzi wa Zahanati ya Laroi, wakati akikagua utekelzaji wa miradi inayoendelea kutekelzwa katika halmasahuri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akikagua ujenzi wa Zahanati ya Laroi, wakati akikagua utekelzaji wa miradi inayoendelea kutekelzwa katika halmasahuri hiyo
Mafundi wakiendelea na kazi ya umaliziaji wa zahanati ya Laroi
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi,akikagua ujenzi wa Zahanati ya Laroi, wakati akikagua utekelzaji wa miradi inayoendelea kutekelzwa katika halmasahuri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.