• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DED ARUSHA DC AWATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MISINGI YA UADILIFU, UWAJIBIKAJI NA NA UMAKINI

Posted on: October 21st, 2021

Na.Elinipa Lupembe.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amewataka watumishi wa halmashauri hiyo, kufanyakazi kwa weledi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za utumishi wa Umma, wakisimamia kanunini ya uadilifu, uwajibikaji, umakini na upendo huku msingi wao mkuu ukiwa ni kufanya kazi kama timu.

Mkurugenzi Msumi ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa kikazi na watumishi wa Makao Makuu ya halmashauri, mkutano ambao ni wa kimkakati katika kuboresha hali ya uwajibikaji, utendajikazi na utekelezaji wa majuku kwa kila mtumishi kisekta, mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Mkurugenzi Msumi amewasisitiza watumishi hao, kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kila mmoja kwa nafasi yake na kulingana na taaluma yake aliyoajiriwa nayo, huku kila mtumishi akitambua na kuthamini umuhimu wa  mtumishi mwingine kiseta, jambo ambalo wakifanya kazi kama timu, watafikia maono ya halmashauri hiyo kwa wepesi, maono yanayojibainisha kuwa halmashuri inayoongoza kwa kutoa huduma bora kwa jamii kwa maendeleo endelevu.

"Watumishi wenzangu, Serikali imewaamini, imewapa dhamani ya kuwahudumia wananchi itumikieni serikali hii kwa kila mmoja kutekeleza majukumu yake bila kusukumwa, wahudumieni wananchi kwa kuwa ndio jukumu letu kubwa, tufanye kazi kama timu, kila mtumishi hapa anao umuhimu wake katika kufikia malengo ya halmashauri na serikali kwa ujumla, nguzo zetu ziwe ni uadilifu, uwajibikaji, umakini na upendo katika eneo la kazi, ukiwa mwadilifu, utawajibika kwa umakini, ukiwa na upendo utamthamini mwingine na kufanya kazi kama timu na kufika malengo ya halmashauri yetu".

Amesisitiza Mkurugenzi huyo.Aidha amewasisitiza watumishi hao, kuwahi kazini na kila mmoja kuwa na mpango kazi wake utakaomuongoza kutekeleza majukumu yake ya kila siku pamoja na kufanya tathmini ya utekezaji wa mpango kazi huo, huku  akiwataka kuhakikisha kila mtumishi anajaza fomu za Opras, fomu ambazo ni dira ya utekelezaji wa mpango kazi na tathmini ya uwajibikaji wa mtumishi kwa kipindi cha nusu mwaka mpaka mwaka mzima.

"Kila siku unapokwenda kazini, hakikisha unafahamu unakwenda kufanya nini kwa kuzingatia mpango kazi wako wa siku, na unapoondoka jioni unajipima utekelezaji wako kwa kutathmini yaliyotekelezeka na kama hayajatekelezeka yawekee mkakati wa utekelezaji wake, kwa kufanya hivyo, halmashauri itafikia malengo yake na serikali kwa ujumla, kwa maendeleo ya taifa letu" ameweka wazi Mkurugenzi Msumi.

Wakati huo huo amewataka wakuu wa Idara na Vitengo kuhakikisha wanafanya vikao vya idara na vitengo vyao kama kanuni zinavyoelekeza, na kutoa nafasi kwa watumishi, kuweka wazi changamoto zao ili zitatuliwe ndani ya idara zao kwa wakati na sio kusubiri kutatuliwa na mkurugenzi, huku wakisimamia maadili ya watumishi pamoja na uwajibikaji kwao kwa kutumia hekima, busara na maarifa yatakawezesha wananchi kupata huduma bora kupitia huduma zinazotolewa katika Idara husika.

Hata hivyo watumishi wa halmasahuri hiyo, wamempongeza mkurugenzi huyo kwa kuweka wazi msingi wa utendaji kazi wake na kuahidi kufanya kazi kwa bidii huku wakimuomba kutatua baadhi ya changamoto zinazokwamisha utendaji kazi na uwajibikaji wa haraka katika maeneo yao ya kazi, ikiwemo vifaa vya kufanyia kazi, mazingira rafiki ya kazi pamoja na usafiri wa kuwafikia wananchi katika maeneo yao na kuzitatua kero zinazowakabili wananchi kwa wakati.

Kikao kazi hicho ni cha kawaida ambacho huwakutanisha watumishi hao na mkurugenzi mtendaji, kikiwa na lengo la kukumbushana utekelezaji wa majukumu ya kila mtumishi kisekta, na kujenga uelewa wa pamoja wa namna bora ya kufikia  malengo ya halmashauri, kwa uzingatia maono na dira ya halmshauri katika kujenga taifa la Tanzania.

Arusha DC

KaziInaendelea✍✍✍✍





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.