Na Elinipa Lupembe
Wakulima na wafugaji wametakiwa kutumia fursa ya maonesho ya Nanenane ili kuweza kujifunza mbinu za kilimo kwa kutumia teknolojia rahisi na za kisasa zitakazo muwezesha mkulima na mfugaji kupata mazao mengi zaidi.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, kwenye banda la Kilimo la Halmashauri hiyo, kwa kuwahamasisha wakulima na wafugaji kutembelea banda hilo kujifunza mambo mbalimbali ya kilimo.
Mkurugenai Msumi amesema kuwa, Maenesho ya 8'8 ni fursa kubwa kwa wakulima na wafugaji kuweza kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa pamoja na kupata uelewa wa matumizi ya njia mbadala za uhifadhi wa chakula bila kutumia kemikali pamoja na ufugaji unaoenda sambamba na utunzaji wa mazingira.
"Kupitia mabanda yetu, wapo watalamu wanaotoa elimu bure ya kilimo na ufugaji wa kisasa, matumizi ya teknolojia rahisi, mnyororo wa thamani katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo, namna bora ya uhifadhi wa chakula kuanzia shambani mpaka kumfikia mlaji, hivyo niwatake wananchi kufika kwenye mabanda yetu kujipatia utaalamu huo" Amesisitiza Msumi.
Hata hivyo amewataka vijana kujiingiza kwenye kilimo kwa kuwa
serikali imeongeza bajeti ya Kilimo ili kuwawezesha vijana kujiingiza kwenye kilimo biashara na kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.
Ameongeza kuwa sera ya nchi kupitia wizara ya Kilimo ni kuwawezesha vijana kujiajiri kwenye sekta ya kilimo ili kujikwamua kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi kupitia kilimo.
Naye Afisa Kilimo Halmashauri ya Arusha Bahati Mtweve, amefafanua Wanawake na Vijana ndio msingi imara wa kuhakikisha misingi endelevu ya chakula kuanzia kwenye uzalishaji, uvunaji, uhifahi mpaka kumfikia mlaji na kuwataka wananchi kufika kwenye maenesho hayo kujionea namna vijana na wanawake wanapaswa kufanya kufikia malengo hayo ya serikali.
"Tunataka watu waje wajifunze usalama wa chakula na mifumo bora ya uhifadhi wa chakula kwa kupunguza uhifadhi wa kutumia kemikali ili kuwa na chakula salama kwa afya za wanadamu"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.