Na Elinipa Lupembe
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amewataka wanachi wa halmashauri hiyo kushirikiana kuifanya Arusha DC, kuwa ya kijani kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa kila mkazi kupanda miti.
Mkurugenzi huyo ametoa rai hiyo, wakati wa zoezi la upandaji miti shule ya msingi Bwawani kata ya Bwawani, ikiwa ni siku ya nne ya Kampeni ya upandaji miti, mwaka 2023 katika halmashauri hiyo.
Amefafanua kuwa kama halmashauri tukiweka nia ya dhati, tunao uwezo mkubwa wa kuifanya Halmashauri yetu kuwa ya kijani, kwa kupanda miti kwa wingi kwa kuhusisha kila mtu kuanzia mtoto mpaka mzee.
"Kila mtu kwenye familia akipanda miti mitano kila mwaka na kuitunza vizuri, Arusha itakuwa ya kijani na itarejesha uoto wake wa asili, tuliouharibu, hilo liko ndani ya uwezo wetu, sisi kama Serikali kwa kushirikiana na wadau, tunatoa miti kwenye vijiji vilivyoathirika zaidi, tumieni fursa hiyo" Amebainisha Msumi.
Ameyataja matokeo ya ukame ambayo wanaArusha tumeanza kuyashuhudia ikiwemo upungufu wa mvua, zaidi mvua kunyesha tofauti na msimu, jambo linalosababisha ukame kwenye halmashauri na maeneo mengi katika nchi yetu.
Aidha amewasisitiza wananchi kuona umuhimu wa kampeni hii ya upandaji miti na kufafanua kuwa, kupanda miti ni jambo muhimu lakini kuitunza miti nia jambo muhimu na kubwa zaidi, hivyo kila mtu aliyepanda mti kuhakikisha anautunza ili ukue.
Diwani wa kata ya Bwawani Mhe. Mollel, licha ya kuushukuru uongozi wa halmashauri kwa kuendesha zoezi la upandaji miti katani kwake, ameahidi kushirikiana na viongozi wa vijiji na vitongoji kuhakikisha wananchi wanapanda miti na kuitunza.
Mhe. Diwani huyo amekiri uwepo wa uharibifu wa mazingira uliosababishwa na ukataji miti, lakini amekiri kuwa serikali za vijiji za kata yake, kwa miaka miwili sasa wameanza utatatibu wa usimamizi wa sheria ndogo za utunzaji wa mazingira, licha ya changamoto ya mifugo
"Nikutoe hofu, mkurugenzi na wadau wetu, miti hii tutaendelea kuisimamia na kuhakikisha wananchi wameiotesha kwenye maeneo yao, na kusimamia ukuaji wake, kwa kuwa tunayo sheri ya mtu anayeharibu mti uliopandwa na hata mifugo yake kula miti" . Mhe Diwani
"Mti wangu, Taifa langu, Mazingira yangu, KaziIendelee"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.