• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DED ARUSHA DC SELEMAN MSUMI, AKABIDIHIWA OFISI RASMI.

Posted on: August 18th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi,  amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Kaim Mkurugenzi, ambaye ni Afisa Elimu Msingi wa halmshauri hiyo, Mwl. Hossein Mghewa.

Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ofisi ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, ambapo aliyekuwankaim mkurugenzi amemkabishi mkurugenzi huyo, kabrasha lenye taarifa iliyosheheni mpango wa shughuli za utekelzaji wa halamashauri ya Arusha, huku Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Mheshimiwa Ojung'u Salekwa akishuhudia zoezi hilo maalum la makabidhiano.

Hata hivyo Mkurugenzi Msumi, amepokea kijiti hicho cha kuingoza halmshauri ya Arusha kwa kuweka wazi vipaumbele vyake ikiwa pamoja na kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuwapa fursa kushiriki na kufahamu huduma zinazotolewa na halmàshauri pamoja na mambo yanayoendelea katika halmashauri yao.

"Ni haki ya kila mwananchi wa halmashauri ya Arusha, kufahamu huduma zinazotolewa na halmashauri ya pamoja na kupata habari za mambo yanayofanyika kwenye halmashauri yao, kupitia tovuti ya halmashauri na kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, hivyo, habari katika channel hizo zote zinatakiwa kuuhishwa mara kwa mara" ameeleza Mkurugenzi Msumi.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha mheshimiwa Ojung'u Salekwa licha ya kumpongeza mkurugenzi huyo kwa kuteuliwa kuingoza halmashauri ya Arusha, amemuhakikishia kuwa ameipokea halmashauri hiyo ikiwa ni salama yenye watumishi  wanaojituma katika kazi, na kumuahidi kushirikiana nae katika kutekeleza  mipango na mikakati ya halmashauri kupitia miradi katika sekta zote, iliyo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Aidha Mheshimiwa Salekwa hakusita kumpongeza aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mwl. Mgewa kwa kuongoza halmashauri kwa kipindi chote ambacho alikaimishwa ofisi hiyo, kwa kuwa hakuwahi kutetereka.

Naye Afisa Elimu Msingi mwl. Mghewa mara baada ya kukabidhi kijiti hicho, ameishukuru familia yote ya halmashauri ya Arusha, ikiwemo Mwenyekiti wa halmshauri, Baraza la Waheshimiwa Madiwani, timu nzima ya menejimenti, watumishi wote, wadau wa maendeleo pamoja  na wananchi  wa halmashauri hiyo kwa ushirikiano mkubwa, waliompa katika kipindi chote cha kukaimu kwake, ofisi hiyo ya mkurugenz.

Hata hivyo amewataka kumpa ushirikiano huo huo Mkurugezni Mtendaji aliyeteuliwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza halmashauri hiyo.Mkurugenzi Msumi anakuwa Mkurugenzi wa sita kuiongoza halmashauri ya Arusha tangu kuanzishwa kwake Julai 2007, baada ya kugawanywa iliyokuwa halmashauri ya wilaya ya Arumeru na kupata halamsahuri mbili za Arusha  na Meru zote zikiwa katika wilaya ya Arumeru

.**TUNAMTAKIA KILA LENYE KHERI MKURUGENZI MSUMI**

ARUSHA DC

KAZI INAENDELEA..✍✍


Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi (kushoto) akipokea kabrasha lenye taarifa za halamshauri hiyo kutoka kwa aliyekuwa kaimu mkurugezi Mwl. Hossein Mghewa.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa (kulia)  akimkabidhi kabrasha lenye taarifa za halamshauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.