Na. Elinipa Lupembe
# Amewataka kufanya kazi kwa kushirikiana kama timu na kuwa na uelewa wa pamoja, juu ya mkakati wa kuendeleza elimu ndani ya hamashauri kwa kuzingatia dira ya halmashauri ya kutoa huduma bora kwa jamii.
# Amewapongeza kwa kazi nzuri iliyowezesha ongezeko kubwa la ufaulu wa wanafunzi katika halmashauri ya Arusha, kutokana na matokeo ya kidato cha pili kwa kufaulu kwa asilimia 90% na kushika nafasi ya 50 kitaifa kutoka nafasi ya 87 mwaka 2017 huku ufaulu wa darasa la nne ukiwa wa asilimia 97.3% na kushika nafasi ya 33 kitaifa kutoka nafasi ya 60 mwaka 2017 wakati darasa la saba wakifaulu kwa asilimia 75% na kushika nafasi ya 21 kitaifa kutoka nafadi ya 91 mwaja 2017 na kuongoza kimkoa ikiwa ni mafanikio makubwa kwa jamii ya wana halmashauri ya Arusha.
# Pia amewapongeza wadau wote wa maendeleo waliojitokeza kuwezesha sekta ya elimu, kwa kazi nzuri walioifanya iliyofanikisha halmashauri kufikia mafanikio hayo makubwa na kuwataka waendelee kujitoa kuunga mkono juhudi za serikali ili kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi na kufikia asilimia 100%.
# Amewataka waratibu wa elimu kata zote kuwa na taarifa sahihi na zenye uhalisia zinazohusu shule zote ndani ya maeneo yao, ikiwemo, ikwemo idadi ya wanafunzi, idadi ya waalimu waliopo na upungufu, idadi ya vyumba vya madarasa, vyoo, ofisi za walimu, maabara na upungufu wake, pamoja na hali halisi ya miundombinu katika shule zote.
# Amewataka kushirikiana na viongozi wa kata na vijiji, kuweka mikakati ya kutatua changamoto zinazozikabili shule katika maeneo yao, hasa katika kuboresha ikiwemo miundombinu ya shule pamoja na kubuni mbinu rafiki zitakazo saidia katika ufundishaji na kujifunza kwa kuwaweka karibu walimu na wazazi.
# Amewataka Maafisa Watendaji wa Kata na vijiji kushiriki, kusimamia sekta ya elimu kwa kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule , pamoja na kuchangia chakula cha watoto wao kwa shule za kutwa.
# Amewataka Maafisa Elimu kata kuzifuatilia shule ambazo hazikufanya vizuri kwenye mtihani yote ya kitaifa na kubaini changamoto zinazozikabili na kuja na mkakati wa kupandisha ufaulu wa shule hizo.
# Wazazi wa maeneo husika wanatakiwa kutambua kuwa shule hizo ni mali yao na wanapaswa kufahamu changamoto za elimu katika maeneo yao na kujitoa kuchangia utatuzi wa changamoto hizo.
# Amemuagiza Mkaguzi wa ndani, kufanya ukaguzi kwenye shule shule ili kubaini changamoto zinazokabili shule na kuzitatua kwa haraka.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.