Na Elinipa Lupembe.
Diwani wa kata ya Matevesi, Mhe. Freddy Lukumay (CCM), amekuwa Makamu Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, mara baada ya kuchaguliwa kwa kura 28 za ndiyo kati ya kura 29 wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani la kufunga mwaka wa fedha 2022/2023
Akitangaza matokeo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, halmashauri ya Arusha, Monica Mwailolo, amesema kuwa kwa kuwa hakuna jina la mgombea mwingine lililowasilishwa hivyo Kwa mujibu wa Kanuni ya 9 (4) ya Kanuni za Kudumu za Halmashauri 2013; iwapo wakati wa kumchagua Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti jina moja tu limependekezwa, wajumbe watapiga kura za Siri za "ndiyo" au " hapana" na endapo kura za "ndiyo" zitazidi asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa basi mgombea atatangazwa kuwa mwenyekiti au makamu Mwenyekiti.
Aidha baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika, Mwailolo alitangaza matokeo hayo kuwa, jumla ya wajumbe 29 walipiga kura na kura za ndiyo zilikuwa 28 huku ka 1 ikiharibika, na kumtangaza Mhe. Freddy Lukumay kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha mara baada ya kushinda kwa kura ya ndio, na kuweka wazi kuwa kisheria Makamu mwenyekiti anashika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
"Kwa kuwa hakuna jina la mgombea mwingine lililowasilishwa hivyo kwa mujibu wa kanuni, tutumelazimika kupiga kura ya ndiyo na kwa kuwa amepata zaidi ya 50% ya kura za ndiyo, ninamtangaza Mheshimiwa Freddy Lukumay kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri na atatumikia nafasi hii kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu za Serikali za Mitaa".Amesisitiza Mwailolo
Mhe.Freddy ameshinda kwa kura za ndio, kutokana na kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, na kuchukua nafasi ya Mhe. Selina Mollel aliyehudumu nafasi ya Makamu mwenyekiti kwa kipindi cha mwaka mmoja ulioanzia Julai 2022 na Kuishia Juni 2023..
Hata hivyo Mhe. Freddy, amewashukuru Waheshimiwa Madiwani wenzake kwa kumuamini na kumchagua kushika nafasi hiyo kwa mara ya pili katika Baraza hilo na kuahidi kushirikiana na Mwenyekiti na uongozi mzima wa halmashauri kwa kuhakikisha mipango na uteklezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo zinasimamiwa vizuri kwa maslahi mapana ya wananwana.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.