• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DIWANI KATA YA MOIVO MHE. SELINA MOLLEL AWA MAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA ARUSHA

Posted on: August 13th, 2022

Na Elinipa Lupembe

Diwani wa kata ya Moivo, Mhe. Selina James Mollel (CCM), amekuwa Makamu Mwenyekiti halmashauri ya Arusha mara baada ya kuchaguliwa kwa kura za ndio wakati wa mkutano maalumu wa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, alimtangaza mheshimiwa Selina Mollel kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha mara baada ya ya kushinda kwa kura ya ndio,  na kuweka wazi kuwa kisheria Makamu mwenyekiti anashika nafasi hiyo kwa kipindi chanmwaka mmoja.

"Kwa kuwa hakuna jina la mgombea mwingine lililowasilishwa tutmelazimika kupiga kura ya ndiyo na kwa kuwa hakuna mjumbe aliyesema hapana, ninamtangaza Mheshimiwa Selina Mollel kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri na atatumikia nafasi hii kwa mujibu wa sheria,,kanuni na taratibu".Amesisitiza Mwenyekiti huyo

Mhe.Selina ameshinda kwa kura za ndio, kutokana na kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, na kuchukua nafasi ya Mhe. Fredi Lukumay aliyehudumu nafasi ya Makamu mwenyekiti kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu tangu baraza hili lianze kazi mwaka 2020.

Mheshimkwa Selina, amewashukuru madiwani wenzake kwa kumuamini na kumchagua kushika nafasi hiyo na kuahidi kushirikiana na Mwenyekiti na uongozi mzima wa halmashauri kwa kuhakikisha mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo zinasimamiwa vizuri kwa maslahi mapana ya wananchi.

Aidha Makamu Mwenyekiti huyo,  amempongeza Makamu Mwenyekiti aliyetangulia kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya na kuwataka waheshimiwa madiwani kumpa shirikiano wakati wote wa kipindi cha uongozi wake ili kutekeleza majuku yake kwa wepesi ya kuwahudumia wananchi.

Hata hivyo Makamu Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, na Diwani wa kata ya Mateves Mhe. Freddy Lukumay, amempongeza makamu mwenyekiti aliyechaguliwa na kuwashukuru madiwani wote na watalamu kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha uongozi wake na kuahidi kutoa ushirikiano zaidi katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Awali Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu, halmashauri ya Arusha, Elizabeth Ngobei, amewasilisha taarifa na miongozi ya ichaguzi huo kuwa, unafanyika  kwa mujibu wa Sheria za serikali za mitaa sura ya 287 marejeo ya mwaka 2002 na Kanuni za Kudumu za halmashauri, Makamu Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Kamati za Kudumu wanapaswa kuchaguliwa kila baada ya mwaka mmoja.

Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa mwaka, umefanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni za serikali za mitaa, ukiwa na agenda za taarifa za maendeleo za mwaka wa fedha 2021/2022, uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti, uundaji wa Kamati za Kudumu za halmashauri pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa kamati hizo za kudumu.


ARUSHA DC TUPO TAYARI KUHESABIWA

SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022


PICHA ZA MATUKIO MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI


Makamu Mwenyekiti mpya halmashauri ya Arusha, mhe. Selina Molle, akiwashukuru wajumbe wa mkutano wa Baraza la Madiwani, mara baada yankumchagua kushika nafasi hiyo, wakati wa mkutano maalum wa mwaka wa Baraza la mMadiwani, kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.