Kuelekea maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano, wa Tanganyika na Zanzibar 2023, halmashauri ya Arusha, imezindua siku hiyo kiwilaya, kwenye shule ya sekondari Mringa kata ya Oloirieni.
Uzinduzi huo umefanyika kwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Emmanulea Kaganda, kuzindua mradi wa ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa vilivyojengwa kwa shilingi milioni 80 fedha kutoka serikali Kuu, maalum kwa ajili ya kupekea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Diwani wa kata ya Oloirin Mhe. Erick Semboja, ametumia wasaa huo, kuishukuru serikali kwa miradi mingi iliyotolewa kwenye kata yake.
Amesema kuwa, mwaka 2021 tulikiwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa shuleni shule ya sekondari Mringa, lakini kwa miaka miwili mfululizo serikali ilitoa fedha shilingi milioni 280, na kujenha, vyumna 14 vya madara, huku mwaka 2021 vikijengwa vyumba 10 kwa milioni 200 na mwaka 2022 vilijenhwa vyumba 4 vya madarsa kwa gharama ya shilingi milioni 80.
Kiasi hicho cha fedha kimetekeleza ujenzi wa vyumba 14 vya madarasa, ofisi mbili za walimu, meza na viti 700, miundombinu ambayo imewezesha wanafunzi wa kidato cha kwanza, kuanza shule kwa wakati.
"Kwa niaba ya wananchi wa Oloirieni, tunaishukuru na kuipongeza serikali yetu ya awamu ya sita, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia watoto wa kitanzania" Amesisistiza Mhe. Diwani
Awali kukamilika kwa vyumba hivyo vya madarasa, umewezesha kupokea jumla ya wanafunzi 576 kati ya wasichana 342 na wavulana 234 kati ya wanafunzi 728 waliopangiwa shuleni hapo.
Kauli mbiu ya Muungano 2023: "Umoja na mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.