Na Elinipa Lupembe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dr. Festo Dugange, ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inaendana na thamani ya fedha ya Serikali iliyotumika na kuipongeza halmashauri ya Arusha kwa ubunifu uliotumika katika kutekeleza miradi hiyo.
Ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya sekondari kiutu, kituo cha Afya Mwandet, kituo cha afya Oldonyosambu pamoja na hospitali ya Wilaya Oltrumet.
Dr. Dugange amesema kuwa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kiutu unaendana na thamani ya fedha iliyotumika pamoja na ubunifu mzuri wa majengo kutokana na ufinyu wa eneo na kuongeza kuwa hali ya utekelezaji wa miradi hiyo inaridhisha licha ya kuwepo kwa mapungufu machache ya umaliziaji wa baadhi ya majengo.
“Rais Dkt. Samia Suluhu ametoa fedha nyingi kutekeleza miradi hii, hivyo Tutakuwa hatujaitendea haki fedha ya serikali kama miradi hii haitaanza kutoa huduma kwa wakati hivyo, niwatake sasa mkamilishe mapungufu madogomadogo yaliyobaki ili miradi hii ianze mara moja kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.” Amesisitiza Dr. Dugange.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe. Noah Saputu amesema kuwa serikali imesaini mikataba tayari kwa ajili ya kutengeza barabara ya kuingia kituo cha afya Mwandet pamoja na mradi wa maji utakaofika hadi maeneo ya kituo hicho cha afya ili huduma za afya ziweze kupatikana kwa urahisi Zaidi bila changamoto yoyote.
“Tunamshukuru sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ya kipekee anavyotujali sisi wananchi wa Arumeru Magharibi ndio maana analeta fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kama hii ndani ya jimbo letu.” Amesema Mhe. Saputu.
Aidha, mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Arumeru, Mhe. Noel Severe ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha pamoja na viongozi wengine kwa kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi huku akiwataka wataalam wa serikali kuzunguka katika kata zote na vijiji kutekeleza majukumu yao badala ya kukaa ofisini tu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda ametumia fursa hiyo kumuomba Mhe. Naibu Waziri kufikisha salamu za wana Arumeru kwa Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kuwapatia fedha hizo za kutekeleza miradi mikubwa ya Afya na elimu ambayo itaokoa Maisha ya wananchi wengi hasa akina mama na watoto.
“Serikali imefanya sehemu yake, ni jukumu letu sasa wananchi kuitunza na kuilinda miundombinu hii ili iweze kunufaisha vizazi vya sasa na baadaye ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kuiboresha pale itakapohitajika.” Ameongeza Mhe. Kaganda.
Awali, wananchi wa maeneo hayo wamemshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa miradi hiyo mikubwa ambayo itaondoa changamoto iliyokuwepo ya elimu na huduma za afya na kumuomba Mhe. Naibu Waziri kuwasadia kutatua changamoto ya maji na barabara ambazo zinawakumba wananchi wa Kata za Mwandet na Oldonyosambu.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#kaziinaendelea✍✍✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.