Na. Elinipa Lupembe
Elimu juu ya ukatili wa kijinsia na maendeleo ya kiuchumi, inayotolewa na shirika lisilo lisilo la kiserikali la DSW, kwa vikundi vya vijana, imewezesha vijana halmashauri ya Arusha, kubadili fikra na mitazamo juu ya mila na desturi potofu zinazodumishwa kwenye jamii yao, pamoja na kupunguza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto..
Elimu hiyo, inayotolewa na mradi wa vijana unaotekelezwa na shirika la DSW, uliotekelezwa kwa miaka miwili sasa, kwenye kata nne za halmashauri hiyo, ukilenga kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia uwezeshaji vijana kiuchumi kwa njia ya vikundi, imeleta mabadiliko chanya na kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Vijana hao wamekiri wakati wa mkutano wa tathmini ya mradi, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuwa, kupitia mradi huo, wameweza kufunguka na kujitambua, kutambua nafasi na wajibu wao katika jamii, kujikwamua kiuchumi kupitia miradi waliyowezeshwa na shirika, jambo ambalo limeleta mabadiliko chanya kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Luciana Saitabau, Mwenyekiti wa kikundi cha TUWEZESHANE kilichopo kijiji cha Olchorovus kata ya Musa, amethibitisha kuwa, kupitia mradi wa shirika la DSW, vijana wamenufaika kwa kupata mbinu na maarifa juu za kujikwamua kiuchumi, sambamba na kupambana na ukatili wa kijinsia unaotokana na mila na destiri za jamii yao.
Amefafanua kuwa, kabla ya mradi haikuwa rahisi, mtoto wa kike kuchanganyika na vijana wa kiume, kujadili nafasi na wajibu wa kijana katika jamii, wala kufanyakazi za uzalishaji kwa pamoja, lakini mradi umeweza kubadili mitazamo hiyo.
"Niweke wazi kuwa, WSD imeleta mabadiliko chanya kwenye jamii yetu, kupiti vijana tuliopata fursa hii, vijana wameweza kutumia maarifa waliyofundishwa kuelimisha jamii yetu kuachana na mila potofu, na mafanikio yameonekana wazi"amesema Luciana
Hata hivyo tathmini ya mradi huo, uliotekelezwa kwa miaka miwi, imeonyesha mafanikio makubwa, kutokana na mradi kuwa shirikishi na kuwapa fursa vijana ya kuoata elimu ya kijamii sambamba na kuwawezesha kiuchumi, kupitia miradi mbalimbali ya ujasiriamali iliyotolewa kwenye vikundi.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii, halmashauru ya Arusha, Beatrce Tengi, amethibitisha kupungua kwa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake kwenye kata hizo 4 kwa mwaka huu.
"Awali kata hizo za Mwandeti, Musa, Olmotony na Sokoni II, zilikuwa na wastani wa matukio 30 kwa mwezi, lakini sasa yamepungu sana mpaka kufikia matukio matatu kwa mwezi" amethibitisha Afisa Ustawi huyo
Naye Mwenyekiti wa kikao hicho na Afisa Maendeleo ya Jamii, halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa, licha ya kulipongeza shirika la DSW, kwa kazi nzuri inayofanyika kwa kipindi cha miaka hiyo miwili, amefafanua kuwa bado kuna changamoto ya ukatili wa kijinsia na ukosefu wa ajira kwa vijana ndani ya halmashauri hiyo, unaotokana na jamii kushikilia mila na desturi zao, pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana.
Ameliomba shirika hilo la DSW, kuangalia uwezekano wa kutekeleza mradi mwingine kama huo kwenye kata nyingine, ili jamii nzima ya halmashauri hiyo, iweze kufikia mpango na sera ya Taifa ya kuwawezesha vijana kiuchumi kuelekea uchumi wa kati na kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Hata hivyo, mkurugenzi wa miradi DSW Tanzania, Peter Owaga, ameishukuru serikali na uongozi wa halmashauri ya Arusha, kwa ushirikiano mkubwa, ulifanikisha utekelezaji wa mradi huo, na kuwasihi vijana kuendeleza maarifa waliyoyapata kwa kwa vijana wengine na jamii kwa ujumla licha ya kuwa ufadhili wa mradi huo kufikia ukomo.
"Naomba mfahamu kuwa, mradi haujaisha, maarifa mliyoyap9ata ndio mradi wenyewe, tumieni maarifa hayo, kurlimisha vijana wenzenu na jamii licha ya kuwa ufadhili umefikia ukomo"amesema Owaga
Jumla ya vikundi 7 vyenye takribani vijana 100 wa kata za Musa, Mwandeti, Olmotony na sokon II, wamenufaika na mradi huo, ulidumu kwa miaka miwili sasa na unategemea kukamilika mapema mwezi Juni 2020.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana cha TUWEZESHANE, Luciana Saitabau, akielezea wajumbe wa kikao, namna mradi wa DSW ulivyowanufaisha vijana wa kata ya Musa.
Msimamivi wa Vikundi vya Vijana ngazi ya jamii 'Kinara' Herieth Solomon, akielezea wajumbe wa kikao, namna mradi wa DSW ulivyoleta mabadiliko kwa vijana na jamii.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.