• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Dtk. PHILIP MPANGO AITAKA TBA KUANZA KUJIEGEMEA

Posted on: August 4th, 2023

Na Elinipa Lupembe

Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameiutaka uongozi wa Wakala wa Majengo nchini - TBA kujipanga kujietegemea katika kuendesha miradi yake na sio kutegemea ruzuku kutoka serikalini.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuzindua  jengo la makazi la kibiashara lililojengwa eneo la Sekei jijini Arusha na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuziwezesha Taasisi zake kuwa na miradi mikubwa itakayowapa uwezo wa kujitegemea na kujiendesha yenyewe.

Aidha Dkt. Mpango amebainisha kuwa, Serikali imeiruhusu Wakala wa Majengo Nchini (TBA) kushirikiana na sekta binafsi kwa ubia ili kuipa fursa na uwanda mpana wa kutekeleza miradi ya kimkakati yenye tija na kuleta matokeo kwa haraka, itakayopunguza hali ya utegemezi kwa Serikali.

“TBA mmefanya kazi nzuri, mmejenga jengo zuri na la kisasa, kuweni na mipango endelevu ya kujenga majengo ya aina hii katika maeneo mbalimbali nchini, majengo yenye uwezo wa kuhudumia kaya nyingi zaidi kwa kuzingatia uwezo wa wananchi, uhifadhi wa mazingira, pandeni miti na maua pamoja na kuweka mifumo mizuri ya maji safi na maji taka’ amesisitiza Dkt. Mpango.

Hata hivyo ameitaka TBA kusimamia vema upangishaji wa nyumba hizo, na kuhakikisha wapangaji wanalipa kodi kwa wakati kulingana na mikaba, ili kufikia malengo ya uzazilishaji utawezesha majengo kujiendesha kibisahara na kuzalisha faida iliyokusudiwa na serikali na kuitaka Wizara ya Uwekezaji kuhakikisha inaweka msukumo kwenye ujenzi wa viwanda wa vifaa vya ujenzi, utakaopunguza gharama za ujenzi ili kuiwezesha Serikali kufikia lengo la ujenzi wa nyumba zitakazoendana na mahitaji ya ongezeko la idadi ya watu.


Naye Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema kuwa azma ya ujenzi huu ni chimbuko la TBA la kutaka kujiendesha  kibiashara kwa kupata faida, hivyo imejipanga kuimisha uanzishaji wa miradi ya kimkakati yenye uwezo wa kujiendesha yenyewe na kuimarisha mfumo wa ukusanyaji kodi.

"Tumeweka mfumo wa kisaa wa vitasa janja ili kudhibiti wapangaji wadanganyifu na wenye madeni, mfumo utakaosaidia ulipaji wa kodi kwa wakati, lengo likiwa ni kupata mapato zaidi na kujiendesha yenyewe." amesisitiza Prof. Mbarawa.

Hata hivyo Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, ameipongeza TBA kwa kujenga majengo marefu yanayodhimibiti matumizi bora ya ardhi na kuhudumia idadi kubwa ya watu na kusisitiza kuwa majengo hayo yaendane na uwepo na maegesho ya magari.

Aidha amebainisha kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa makazi nchi, na kuweka wazi kuwa zaidi ya 390,981 zinahitajika kwa mwaka ukilinganisha na idadi ya chini ya nyumba 2000 zinazojengwa na taasisi mbalimbali kwa mwaka.

#KaziInaendeela




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.