Na Elinipa Lupembe.
Watu mbalimbali wamejitokeza kutembelea banda la Kilimo halmashauri ya arusha kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini eneo la Themi Njiro Jijini Arusha.
Afisa Kilimo Charles Leseiyo, akiwaelezea fursa adhimu inayotolewa na serikali kwa wakulima kwa kuwakopesha Matreka kupitia Mfuko wa Pembejeo za kilimo..
Serikali kupitia halmasahuri ya Arusha inawawezesha wakulima kutumia teknolojia za kisasa katika kilimo ili kufikia Ajenda 10-30 ya Kilimo Biashara.
Aidha Lesiyo amewata wakulima wote, kufika kwenye banda la kilimo na hatimaye kufika kwenye ofisi za Halmashauri ya Arusha kujipatia fursa hiyo ya Mikopo yenye riba nafuu ambayo kila mkulima wa kitanzania anauwezo wa kumudu ili kufikia malengo.
Tembelea Mabanda ya Kilimo na Mifugo, halmasahuri ya Arusha, kujifunza teknolojia za kisasa za Kilimo na Mifugo ili kufikia Ajenda 10 - 30 ya Kilimo Biashara.
Kauli Mbiu ya Nanenane 2022: "AJENDA YA 10 -30 KILIMO NI BIASHARA 'SHIRIKI KUHESABIWA KWA MIPANGO BORA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.