Na Elinipa Lupembe
Lengo la Sensa ya watu na makazi ni kupata taarifa sahihi za Kidemografia, Kijamii, Kiuchumi na Mazingira kwa lengo la kupata Takwimu sahihi zitakazoiwezesha Serikali na wadau wengine kupanga kwa usahihi mipango ya maendeleo ya watu wake katika sekta mbalimbali za elimu, afya, hali ya ajira, miundombinu kama barabara, nishati na maji safi.
Kwa msingi huo, Sensa ni zoezi muhimu ambalo kila mmoja kwa nafasi yake analazimika kushiriki na kutimiza wajibu wake ili kuhakikisha Sensa ya Watu na Makazi 2022, inakuwa ya mafanikio makubwa.
Hii itasaidia Serikari kutimiza wajibu wake kwa wananchi kulingana na idadi ya watu ya eneo husika ikiwa kama msingi mkubwa wa ugawaji wa keki ya taifa kwa kila eneo la utawala hapa Nchini.
"Sensa ni Msingi wa Mipango Bora ya Utumishi wa Umma, Ewe Mtumishi wa Umma Hakikisha Umehesabiwa" AFISA UTAWALA NA RASILIMALI WATU ARUSHA DC, Elizabeth Ngobei
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.