FAHAMU NANI ANAPASWA KUHESABIWA
Na Elinipa Lupembe
Katika Sensa ya mwaka 2022 kama zilivyo Sensa zilizopita, itafanyika Nchi nzima na itahusisha watu wote watakaolala ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hii inamaanisha kuwa, watu wote watakaolala katika kaya binafsi usiku wa kuamkia siku ya Sensa.
Watu wote watakaokuwa katika kaya za jumuiya kama vile Hotelini, nyumba za kulala wageni, Hospitalini, Magereza, Mabweni ya wanafunzi, kambi za Jeshi, vituo vya kulelea watu wenye mahitaji maalum kama yatima na wazee, kambi za wavuvi, watu wasio na makazi maalum na vituo vya usafiri wa umma (kama vituo vya mabasi, garimoshi, viwanja vya ndege na bandari) watahesabiwa kwa kutumia utaratibu maalum utakaoandaliwa na kamati ya za Sensa katika ngazi ya Mtaa, Kitongoji na Shehia.
"Tambua kuwa kila mtu ana Haki ya Kuhesabiwa, Sensa ni Msingi Bora wa Upatikanaji wa Haki na Usawa" Monica Mwailolo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria ARUSHA DC
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
JIANDAE KUHESABIWA✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.