Na Elinipa Lupembe
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Arumeru, Peter Maina, amesema kuwa serikali inaendelea kutoa fedha za upanuzi wa miradi ya miradi ya maji ambayo imeanza ili kufikia maeneo ambayo hayajafikiwa na hudumza ya maji.
Maji yamefika kijiji cha Lesiraa lakini kuna baadhi ya maeneo hayajafika hususani kitongoji cha Bwawani, kadri fedha zitakavyotolewa na serikali mradi huo utapanuliwa ili kuwafikia wananchi wa kitongoji hicho cha Bwawani
Maina ametoa ufafanuzi wakati akijibu swali lilioulizwa na Diwani wa Kata ya Kisongo aliyeomba ufafanuzi wa hatma ya mradi wa maji Lesira kwa kuwafikia wanachi wa kitongoji cha Bwawani kilichopo ndani ya kijiji hicho, wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Taarifa za robo ya Julai - Septemba 2022.
Hata hiyo Maina amesema kuwa serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ukamilishaji na upanuzi wa miradi ya maji ambayo imeanza ili kufikia maeneo ambayo hayajapata huduma za maji.
Akiwasilisha taarifa yake Kaimu Meneja huyo amebainisha kuwa, katika kipindi cha robo ya kwanza RUWASA imenelea kutekelza miradi ya maji kupitia fedha za Mfuko wa Maji (NWF), Fedha za UVIKO 19 na fedha za malipo kwa matokeo (PbRV).
Aidha amefafanua kiasi cha shilingi milioni 801.1 za NWF, zinatekeleza mradi wa maji Losikito kukiwa na ujenzi wa nyumba ya pumpu, tanki la kukusnayia maji na uzio, huku milioni 376 za PbRV zikitekeleza mradi wa maji Manyire, Marurani na Majimoto shilingi milioni 200 na mradi wa maji Old Nduruma kwa shilingi milioni 176 na yote imefikia asilimia 90 ya utekelazaji wake.
ARUSHA DC
KaziInaendelea ✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.