MAELEKEZO YA UCHAGUZI KATIKA MAMLAKA ZA WILAYA
(Yametolewa chini ya Kanuni ya 9)
Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kijiji Na.373 Kanuni ya 9(1) kinachoeleza kuwa Msimamizi wa Uchaguzi atatoa maelekezo ya Uchaguzi; Hivyo basi:
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika tarehe 24.11.2019.
Uandikishaji utafanyika tarehe 8 hadi 14 Oktoba, 2019 katika Vitongoji 238 na Vijiji 67 vya Halmashauri ya Arusha ambapo kutakuwa na vituo 238 vya kuandikisha Wapiga Kura vitakavyofunguliwa saa mbili kamili asubuhi (02.00) na kufungwa saa kumi na mbili kamili jioni (12.00)
Uchaguzi utafanyika tarehe 24 Novemba, 2019 katika Vitongoji 238 na Vijiji 67 katika Halmashauri ya Arusha ambapo kutakuwa na vituo 238 vya Kupiga Kura vitakavyofunguliwa saa mbili kamili asubuhi (02.00) hadi saa kumi kamili jioni (10.00).
Nawasisitiza Wakazi wote wenye sifa za kupiga kura kujiandikisha ili kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 24.11.2019.
Nawasisitiza wakazi wenye umri wa miaka ishirini na moja au zaidi wanaotaka kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kitongoji, Mwenyekiti wa Kijiji, na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, kuchukua fomu za kugombea zitakazopatikana kwenye ofisi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
Fomu za maombi ya kugombea Uenyekiti wa Kitongoji, Wajumbe wa Halmashauri na Wenyeviti zitachukuliwa tarehe 29.10.2019 saa moja na nusu asubuhi (01.30) na kurejeshwa tarehe 04.11.2019; Mwisho wa kupokea fomu ni saa kumi kamili jioni (10.00). Fomu hizo zitatolewa kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
Siku ya Uteuzi wa Wagombea ni tarehe 05.11.2019, na fomu za wagombea zitabandikwa kwenye mbao za matangazo.
Uwasilishaji wa Pingamizi dhidi ya uteuzi wa Mgombea yeyote ni kuanzia tarehe 05 hadi 06.11 2019 na uamuzi wa Pingamizi kuhusu uteuzi wa Mgombea ni tarehe 05 hadi 07.11.2019.
Rufaa dhidi ya uamuzi wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ni tarehe 05 hadi 08.11.2019.
Mikutano ya Kampeni itakua siku saba na itaanza tarehe 17.11.2019 hadi 23.11.2019 ambapo itaanz saa mbili asubuhi (02.00) na itamalizika saa kumi na mbili jioni (12.00) ya kila siku ya Kampeni.
Nawasisitiza wananchi kushiriki Uchaguzi kwa wingi, wapige kura kwa amani. Kulingana na Kanuni ya 35(6) mtu yeyote hatoruhusiwa kubaki katika eneo la kituo cha kupiga kura baada ya kupiga kura.
MAELEKEZO YA UCHAGUZI KWA MAMLAKA YA MJI MDOGO NGARAMTONI
(Yametolewa chini ya Kanuni ya 8)
Kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Mji Mdogo Na.371 (2019) kifungu cha 8(1) kinachoeleza kuwa Msimamizi wa Uchaguzi atatoa maelezo ya Uchaguzi; Hivyo basi:
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika tarehe 24.11.2019.
Uandikishaji utafanyika tarehe 8 hadi 14 mwezi Oktoba, 2019 katika Vitongoji 21 vya Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramatoni ambapo kutakuwa na vituo vya uandikishaji 42 vitakavyofunguliwa saa mbili kamili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili kamili jioni.
Uchaguzi utafanyika tarehe 24 Novemba, 2019 katika Vitongoji 21 vya Mamlaka ya Mji Mdogo ambapo kutakuwa na vituo 42 vya kupigia kura vitakavyofunguliwa saa mbili kamili asubuhi mpaka saa kumi kamili jioni.
Nawasisitiza Wakazi wote wenye sifa za kupiga kura kujiandikisha ili kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 24.11.2019.
Nawasisitiza wakazi wenye umri wa miaka ishirini na moja au zaidi wanaotaka kugombea nafasi ya uenyekiti wa Kitongoji kuchukua fomu za kugombea zitakazopatikana kwenye ofisi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
Fomu za maombi ya kugombea Uenyekiti wa Kitongoji zitachukuliwa tarehe 29.10.2019 saa moja na nusu asubuhi (01.30) na mwisho wa kurejeshwa fomu ni tarehe 04.11.2019 saa kumi kamili jioni (10.00. Fomu hizo zitatolewa kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
Siku ya Uteuzi wa Wagombea itakuwa tarehe 05.11.2019, na fomu za wagombea zitabandikwa kwenye mbao za matangazo ya Vitongoji.
Uwasilishaji wa Pingamizi dhidi ya uteuzi wa Mgombea yeyote ni kuanzia tarehe 05 hadi 06.11 2019 na uamuzi wa Pingamizi dhidi ya uteuzi wa Mgombea ni tarehe 05 hadi 07.11.2019.
Rufaa dhidi ya uamuzi wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ni tarehe 05 hadi 08.11.2019.
Mikutano ya Kampeni itakuwa siku saba na itaanza tarehe 17.11.2019 hadi 23.11.2019 ambapo itaanza saa mbili asubuhi (02.00) na itamalizika saa kumi na mbili jioni (12.00) ya kila siku ya Kampeni.
Nawasisitiza wananchi kushiriki Uchaguzi kwa wingi, wapige kura kwa amani. Kulingana na Kanuni ya 34(6) mtu yeyote hatoruhusiwa kubaki katika eneo la kituo cha kupiga kura baada ya kupiga kura.
Imetolewa na:
Hossein R. Mghewa
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI
HALMASHAURI YA ARUSHA
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Arusha, Mwl. Hossein Mghewa akitoa maelekezo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.