Na. Elinipa Lupembe.
Mkurugenzi mtendaji halmasahuri ya Arusha, Selemani Msumi, amewataka watoa huduma wote, kuendelea kuboresha hali ya utoaji huduma kwa wateja katika taasisi zao, kwa kuwa huduma kwa mteja ndio msingi wa kufikia malengo ya taasisi husika.
Amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja, yaliyofanyika katika benki ya CRDB tawi la Sekei, halmasahuri ya Arusha, wilaya ya Arumeru, na kusisitia kuwa ili taasisi iweze kufikia malengo yake ya kibiashara na kijamii, lazima kipengele cha huduma bora kwa mteja kizingatiwe na kutiliwa mkaźo ili kuweza kumfanya mteja kuelendelea kuiamini taasisi inayomuhudumia.
"Tunafahamu taasisi ni nyingi na zinazotoa huduma zinazofanafa, ili kumpata mteja na kumfanya aendelee kudumu na kuiamini taasisi yako, lazima suala la huduma kwa mteja liwe imara na lenye kupewa kipaumbele, hii itasaidia taasisi kumudu ushindani mkubwa uliopo katika soko" amesisitiza Mkurugenzi huyo.
Naye Meneja wa CRDB tawi la Sekei, Winsara Ndanshau, amesema kuwa benki ya CRDB imeendelea kuwajali wateja wake kwa kutoa huduma bora huku uboreshaji wa huduma kwa mteja ukiwa ni kipaumbe, lengo likiwa kuimarisha uhusiano kati ya benki na mteja.
Winsara amezitaja huduma zinazotolewa na benki hiyo ni pamoja na huduma zote za kibenki, ikiwemo akaunti za akiba, akaunti za watoto 'Junior Jumbo', akaunti maalumu kwa wanawake 'Malkia Akaunti' akaunti za wafanayakazi, wafanyabishara wakubwa na wadogo, mikopo kwa wafanyakazi wa serikalini, wafanyabiashara wakubwa, mikopo kwa wafanya biashara wadogo 'wajasiriamali' mikopo kwa wakulima sambamba na huduma za bima ya maisha, afya, majengo na vyombo vya moto.
Hata hivyo baadhi ya wateja wa CRDB walioshirikia hafla hiyo, baada ya kufika tawini hapa kupata huduma, wameipongeza benki hiyo kwa kutoa huduma bora, huduma ambazo hupatikana kwa wakati pindi mteja anapohitaji, jambo ambalo linawafanya kuendelea kuiamini benki hiyo inayowajali wateja wake.
Ian Cherles mteja wa CRDB tawi la Sekei, ameweka wazi kuwa yeye hufika kwenye tawi hilo mara kwa mara kupata huduma za kibenki na hajawahi kupata mkwamo, na kuongeza kuwa hata pindi inapotokea changamoto yoyote, hupata utatuzi wake kwa haraka na kwa wakati, kutokana na benki hiyo kuwa na huduma bora kwa wateja.
Awali,maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja hufanyika wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka 2021 ni *Nguvu ya Huduma*, huku benki ya CRDB tawi la Sekei ikijumuika na wateja wake, katika hafla fupi ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja katika benki hiyo.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkurugenzi Mtendaji halamshauri ya Arusha ( wa kwanza kushoto) na Meneja wa CRDB tawi la Sekei Winsara Ndanshau, wakikata keki, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Mteja katika tawi hilo la Sekei.
Baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB tawi la Sekei wakipata huduma wakati wa maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Mteja katika tawi hilo la Sekei
Baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB tawi la Sekei wakimsikiliza mgeni rasmi, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Mteja katika tawi hilo la Sekei
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.