• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

IDARA YA MAENDELEO YA JAMII KUTKELEZA MRADI WA TCI- TUPANGE PAMOJA KWA VITENDO

Posted on: September 3rd, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Arusha, imejipanga vema kushiriki katika kutekeleza mradi wa TCI -Tupange Pamoja, kwa kuhamasisha umma kupata elimu ya afya ya uzazi kwa vijana,  kupitia  mpango wa Huduma Rafiki kwa Vijana kupitia makundi maalumu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Afisa Maendeleo ya Jamii, halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa, amesema kuwa, idara yake inashughulika na makundi mbalimbali ya jamii, ameahidi kutumia fursa hiyo kuhamasisha umma, kutekeleza mradi huo wa Tupange Pamoja na Tuwaveshe Salama, mradi unaotekeleza na halmshauri kwa ufadhili wa shirika la JPEIGHO.

Angela amethibitisha, kutumia fursa ya majukwaa hayo, kutoa elimu na kuwahamasisha juu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana pamoja na Upatikanaji wa Huduma rafiki kwa vijana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. 

"Tunakutana na makundi ya Wanawake, Vijana na walemavu kwa ajili ya kutoa elimu ya ujasiriamali na mikopo, tunakunata na makundi ya watoto na vijana wanaoishi kwebpnye mazingira magumu, na pia tuna klabu za watoto shule za msingi na sekondari, kupitia makundi haya elimu ya Afya ya uzazi kwa vijana itafika kwa watu wengi zaidi"  amesema Afisa huyo.

Aidha amefafanua kuwa, taarifa hizi zikiifikia jamii kwa usahihi kupitia  makundi mbalimbali, ni rahisi kuokoa vijana wengi kuingia kwenye ndoa za utotoni, ndoa na watoto wasiotarajiwa  na kuwafanya vijana kujitambua na kutimiza ndoto zao na kuwa na taifa bora lenye watu wenye afya bora.

Hata hivyo Angela amefafanua zaidi kuwa, mtazamo hasi wa jamii yetu, juu ya Afya ya uzazi kwa vijana, unaofanya jamii hasa wazazi kudhani mtoto akijifunza mambo ya uzazi atajiingiza kwenye kwenye vitendo vya ngono.

Ameitaka jamii kuachana na mawazo hayo potofu na kutambua kuwa elimu ya afya ya uzazi ina lengo la kumfanya kijana kutambua mabadiliko ya mwili wake, athari na madhara ya mabadiliko hayo na namna ya kukabiliana na mihemko ya mwili wake, namna ya kujikinga na magonjwa yatokanayo na kujamiiana na jinsi ya kujikinga.


Hata hivyo imefahamika, vijana hawana taarifa sahihi juu ya afya ya uzazi, badala yake hufundishana wao kwa wao na matokeo yake, hujikuta kuanza kujamiiana na kujikuta, wakilazimika kuingia kwenye ndoa za utotoni kutokana na  mimba zisizotarajiwa,  umefika wakati sasa kuwawezesha vijana kupata taarifa sahihi, juu ya afya zao ili kujipanga na kujiandaa na maisha yao ya familia ya baadaye bila kuathiri masomo na mipango ya maendeleo yao.

Huduma Rafiki kwa Vijana, hutoa elimu  ya  Afya ya Uzazi kwa Vijana, na inapatikana kenye vituo vya Afya 15 ndani ya halmashauri ya Arusha, kupitia mradi wa TCI- TUPANGE PAMOJA, mradi uliofadhiliwa na shirika la JHPEIGO.

Afisa Maendeleo ya Jamii, halmashauri ya Arusha, Angela Mvaa akizungumza na Mratibu wa Mradi TCI- TUPANGE PAMOJA, Waziri Njau, namna idara yake itakavyotekeleza mradi wa TCI- TUPANGE PAMOJA na HUDUMA RAFIKI KWA VIJANA.


Afisa M/Jamii, halmashauri ya Arusha akijiunga na kupakua vitini vya masomo TCI-TUPANGE PAMOJA kwenye mtandao. 


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.