Na Elinipa Lupembe
Jamii imetakiwa kuwadhibiti watoto dhidi ya matumizi ya teknolojia ya ya mawasiliano mtandao, ili kukabiliana na ulimwengu wa digitali, teknolojia ambayo imeaminika kuwa na kasi ya kumomonyoa maadili kwa jamii huku watoto wakiwa wakiathirika wakubwa.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya Arumeru Mhe. Emmanula Mtatifikolo Kaganda, wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika halmashauri ya Arusha, zilizofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Loovilukuny Kata ya Kisongo.
Amewataka wazazi kuzingatia usalama wa watoto dhidi ya matumizi ya simu janja, komputa na televisheni kwa kuwa, vifaa hivyo vya kiditali vina mambo mengi mazuri na mabaya, ambapo watoto huvutiwa zaidi na mambo mabaya, ambayo huathiri tabia za watoto kwa kuiga na kufanya mambo hayo katika maisha yao ya kawaida, tabia ambazo ni kinyume na maadili ya jamii za kitanzania.
Amefafanua kuwa, licha ya maadili kumomonyoka kupitia matumizi ya digitali, hatuwezi kuishi nje wala kujitenga nayo, ila wazazi na walezi mnalo jukumu kubwa la kudhibiti na kuwasimia watoto na kuhakikisha wanafanya matumizi salama ya digitali kwa kuzingatia usalama wa mtoto ili kuwaepusha watoto na madhara yanayotokana na mambo mengi yanayopatikana mtandaoni.
"Wazazi tusione sifa watoto kuiga tabia za kimagharibi, tutunze tamadumi zetu, jukumu letu kubwa ni kuhakikisha maisha ya watoto yanakuwa salama kwa kuwa digitali ndio mfumo wa maisha ya sasa, hutuwezi kujitenga nao, la msingi ni wazazi na wadau kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha watoto wetu wawe salama kupitia uwepo wa digitali katika maisha yetu" Amesisitiza Mhe. Emmanuela.
Awali wakisoma risala, watoto wamelalamikia matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kusababisha vitendo vya ukatili vinavyofanyika dhidi ya watoto huku watoto wakifanya ngono katika umri mdogo huku wengine wakilawitiana wenyewe kwa wenyewe na kuwaomba wazazi, walezi na mamlaka za serikali kusimamia maadili ya mitandaoni.
"Watoto tunasikitishwa sana vitendo vibaya vinavyofanywa na watoto, kutokana na matumizi ya mitandao ya mawasiliano, kumekuwa na wimbi la watoto kujiingiza kwenye ngono, katika umri mdogo huku wengine wakilawitiana wenyewe kwa wenye, tunaomba serikali kusimamia maudhui ya watoto mitandaoni" Ameweka wazi msoma Zenufa Said
Hata hivyo wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto (MTAKUWWA) kijiji cha Loovilukuny wamethibitisha tabia ya wazazi kwa kisasa kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii na kutelekeza majukumu yao ya kusimamia watoto, jambo ambalo linaathiri sana tabia za watoto.
"Baba na mama wako bize kwenye simu zao, wakiwaacha watoto wakiangalia katuni na michezo mingi kwenye mtandao, tabia ambazo zimeongeza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto ni vyema wazazi kurejea kwenye mstari wa malezi.
Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya mtoto, imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika 2023 yenye Kauli Mbiu ya "Zingatia Usalama wa Mtoto katika Ulimwengu wa Kidigitali"
ARUSHA DC Ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.