• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

JAMII YATAKIWA KUACHA FIKRA POTOFU JUU CHANJO NA DAWA TIBA ZINAZOTOLEEWA NA  SERIKALI

Posted on: November 23rd, 2022

Na Elinipa Lupembe.

Jamii imetakiwa kuachana na dhana potofu za kudhani kuwa chanjo na kinga tiba zinazotolewa na serikali zina madhara kwa afya ya binadamu na kushawishi wengine kukataa.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa, wakati akizindua zoezi la kitaifa la umezeshaji vidonge vya kinga tiba dhidi ya minyoo tumbo kwa watoto wa umri wa miaka 5 mpaka 14 halmashauri ya Arusha, uzinduzi uliofanyika kwenye shule ya msingi Olgilai kata ya Kiutu.

Mhe. Ojung'u amesema kuwa chanjo na kinga tiba zinazotolewa na serikali zikiwa zimepimwa na kuthibitishwa kuwa na viwango vya ubora kwa binadamu zaidi ni salama kwa afya za binadamu.

"Serikali inathamini afya za watanzania, na inaweka mipango thabiti ya kuwakinga wananchi hususani watoto dhidi ya magonjwa ambayo yana kinga, kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba".Amesema Mhe. Mwenyekiti.

Katika zoezi hilo Diwani wa kata ya Kiutu, ameishukuru serikali kwa kutoa kinga tiba hiyo ambayo inawakinga  watoto dhidi ya minyoo tumbo ambayo ina madhara makubwa kwa afya ya binadamu hususani watoto.

Mganga Mkuu halmashauri ya Arusha, Dkt. Petro Mboya, amesema kuwa vidonge vinavyotolewa ni almebendazole ambavyo hukinga dhidi ya minyoo tumbo na hutolewa kwa watoto kwa sababu wako kwenye hatari ya kupata mayai ya minyoo kutokana na tabia za michezo ya watoto.

"Tunatoa kinga tiba kwa watoto wa miaka 5 mpaka 14 kwa kuwa wako kwenye hatari ya kupatwa na mayai ya minyoo, kutokana na uwezo wao mdogo wa kujikinga na uchafu, watoto wengi hushindwa kunawa mikono na hula bila kunawa mikono na wakati mwingine huokota vitu na kula". Amebainisha Dkt. Mboya

Mwalimu mkuu shule ya Msingi Oligilai, Mwl. Recho Kisiri, amesema kuwa, wanafunzi wamehudhuria masomo kwa wingi wao na wanategemea kumezesha dawa za minyoo takriban watoto 782 na kufikia asilimia 100.

Hata hivyo mratibu wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele, Halmashauri ya Arusha, Ramadhani Kulewa, amesema kuwa, dawa tiba hiyo inatolewa kwenye vituo 211, shule za msingi 155, vituo vya afya 56, huku wahudumu 433 wakigawa dawa hiyo ambapo walimu ni 310 na wahudumu wa afya 112.

Awali Halmashauri inategemea kuwapatia kinga tiba ya minyoo kwa watoto elfu 80, watoto elfu 76 kati yao ni wale waliosajiliwa shuleni na watoto elfu 4 ni ambao hawajasajiliwa kwenye mfumo rasmi wa elimu.


ARUSHA DC

KaziInaendelea✍


Mwenyekiti halmashauri ya Arusha Mhe. Ojung'u Salekwa, akimmezesha dawa mwanafunzi wa shule ya msingi Olgilai, wakati wa kuzindua zoezi la chanjo ya kinga tiba ya minyoo tumbo



Diwani wa kata ya Kiutu Mhe. Malaki Malambo, akimmezesha dawa mwanafunzi wa shule ya msingi Olgilai, wakati wa kuzindua zoezi la chanjo ya kinga tiba ya minyoo tumbo




Afisa Mipango Msaidizi Kitengo cha Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele Wizara ya Afya Dkt. Dorca Burengelo, akimmezesha dawa ya minyoo mwanafunzi wa shule ya msingi Olgilai kata ya Kiutu, wakati wa  uzinduzi wa zoezi la Kitaifa la kumezesha dawa za kinga tiba dhidi ya Minyoo halmashauri ya Arusha.



Mganga Mkuu, Halmashauri ya Arusha, Dkt. Petro Mboya akimmezesha dawa ya minyoo mwanafunzi wa shule ya msingi Olgilai, wakati wa  uzinduzi wa Zoezi la kitaifa la kumezesha dawa za kinga tiba dhidi ya Minyoo halmashauri ya Arusha.












Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.