• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA SUALA LA MALEZI PASIPO KUBAGUA JINSIA YA WATOTO

Posted on: October 12th, 2023

Mwenyekiti wa Halmshauri ya Arusha Mhe. Dkt.Ojung'u Salekwa ameitaka Jamii ya Watanzania kuendelea kushirikiana katika suala malezi ya watoto pasipo kubagua jinsia ya mtoto ili kuwa na Taifa lenye Afya.

Amezungumza hayo leo wakati wa kikao kazi cha Wadau kilichoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Center For Women and Children Center (CWCD) katika mradi wake wa kuwawezesha Watoto wa Kiume dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Dkt.Salekwa amesema kuwa, jamii ya kitanzania lazima ichukue hatua za makusudi katika suala la malezi ya watoto kwani takwimu zinaonyesha kuwa wazazi wengi wamekuwa wakiwaacha watoto kujiamulia mambo yao wanavyotaka pasipo kukemewa.

"Utakuta mtoto mbele ya wazazi wake anavaa mavazi yasiyo na staha, lakini hakemewi na wazazi wanaona ni kwenda na usasa, hii inatuharibia Taifa kwani watoto hawa ndiyo Viongozi na wazazi wa wakati ujao", amesema.

Akizungumzia mafanikio ya mradi huo, mratibu wa Mradi kutoka Shirika la CWCD Epiphania Josephat amesema kwa kushirikiana na Halmshauri ya Arusha, wamefanikiwa kuanzisha maabara 6 za watoto wa kiume katika Shule za Msingi za Kiranyi, Moivo, Naurei, Ngaramtoni, Ilboru na Oltruroto.  Vilevile wameteua baba waangalizi 6 kwa kila kata, pamoja  na vikundi 6 vya malezi kwa kila Kata.

Kupitia vikundi hivyo, Shirika la CWCD kwa kushirikiana na Halmshauri ya Arusha, wameweza kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo watoto wa kiume ili wajitambua katika kuzijua haki zao pamoja na kuripoti vitendo vyovyote vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea katika jamii wanazotoka.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Halmshauri ya Arusha Beatrice Tengi amesema kuwa, Serikali imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la CWCD katika mpango wa makuzi ya mtoto kuanzia ujauzito mpaka miaka 8 ikiwa ni kumjenga mtoto kimakuzi kwa kuhakikisha mtoto anapata malezi salama ikiwemo elimu bora.

Akifunga Kikao hicho, Mkurugenzi wa Halmshauri ya Arusha DC, Seleman Msumi amesema kuwa, Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha inamlinda mtoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kufungua madawati ya kushughulikia vitendo hivyo ndani ya Jeshi la Polisi.

Vilevile Msumi ametoa wito kwa Viongozi wa Dini, kuendelea kutoa mafundisho katika nyumba za Ibada ili jamii iweze kuwa na hofu ya Mungu, kwani pasipo kufanya hivyo Taifa litakosa nguvu kazi ya baadaye ambayo inategemea sana Vijana.


ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.