Mambo muhimu unayopaswa kuyafahamu kuhusu sensa ya watu na makazi ni yafuatayo;
SENSA YA WATU NA MAKAZI NI NINI?
Sensa ya watu na makazi ni moja ya zoezi muhimu linalokusanya taarifa za kila mtu aliyelala ndani ya mipaka ya Nchi usiku wa kuamkia siku ya Sensa. Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kama zilivyo Sensa zilizopita, itahusisha Makarani wa Sensa ambao watatembelea kaya zote Nchini na kufanya mahojiano ya ana kwa ana baina ya Karani wa Sensa na Mkuu wa Kaya.
Karani wa Sensa atafanya mahojiano na mtu mzima yoyote katika kaya ambaye ana taarifa za kutosha uhusu kaya na wanakaya wenzake waliolala katika kaya husika usiku wa kuamkia siku ya Sensa.
"JIANADAE KUHESABIWA 23.08.2022.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.