Na Elinipa Lupembe
Jumla ya wanafunzi 9,711 wa shule za msingi 141 halmashauri ya Arusha, wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2022 kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa.
Akizungumza na mwandishi wetu, ofisini kwake Mwenyekiti wa kamati ya Mitihani, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amesema kuwa tayari taratibu zote za maandalizi ya mtihani zimekamilika na wasimamizi wote walishapatiwa semina za usimamizi wa mtihani, walimu na wanafunzi wamejiandaa kwa mtihani huo.
Aidha Mkurugenzi Msumi, licha ya kuwatakia kila la Kheri wanafunzi wote wanaofanya mtihani huo, lakini amewataka wasimamizi wote kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Mtihani wa Taifa na kuepuka aina yoyote ya vitendo vya udanganyifu katika mtihani huo kwa kuwa tayari maelekezo yote yameshatolewa.
"Niwatake wasimamizi wote kufuata taratibu, serikali haitavumilia kwa yoyote atakayejihusisha na udanganyifu wa aina yoyote, ninamini wengi wetu ni wazazi, tuwasimamie vizuri na kwa uaminifu watoto hawa wasio na hatia, msiwaangize kwenye matatizo yasiyowahusu" Amesistiza Mkurugenzi Msumi
Naye Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi, Mwl. Salvatory Alute amethibitisha kukamilika kwa taratibu zote za maandalizi ya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na kuweka wazi kuwa jumla ya wanafunzi 9,711 kufanya mtihani huo kwa siku mbili tarehe 05 - 06 Oktoba, 2022.
Aidha Afisa Elimu huyo, ameweka wazi kuwa idadi hiyo ya wanafunzi 9,711 watakaofanya mtihani huo, wavulana ni 4,628 na wasichana 5,083 kutoka shule 141 za msingi, huku shule 93 za serikali na shule 48 za taasisi na zile za binafsi.
Uongozi wa halmashauri ya Arusha, unawatakia kila la kheri wanafunzi wote wanaofanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu darasa la saba 2022, Mwenyenzi Mungu awasimamie.
KILA LA KHERI WANAFUNZI WOTE WANAOFANYA MTIHANI WA TAIFA, MWENYENZI MUNGU AWASIMAMIE
ARUSHA DC
#Kazi Inaendea
Pichani: wanafunzi wa darasa la VII shule ya msingi Oldonyosambu
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.