Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Arusha,Daktari Japhet Champanda amewataka wajumbe wa kikao cha kujadili vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kujikita katika kutafuta suluhisho la kutokomeza vifo vya mama na mtoto katika Halmashauri ya Arusha.
Daktari,Champanda ametoa rai hiyo leo tarehe 9/07/2024 wakati akifungua kikao cha robo mwaka ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024 chenye lengo la kujadili changamoto zinapelekea vifo vinavyotokana na uzazi na watoto wachanga katika jamii kisha kuja na mikakati bora ya kuzuia vifo hivyo.
Akitoa takwimu za kupungua kwa Vifo hivyo,Muunguzi Mkuu wa Halmshauri ya Arusha Bi.Noemi Peter Temu amesema, kwa kipindi cha mwezi januari hadi machi 2024 kulikuwa na vifo 11 vilivyotokana na uzazi na watoto wachanga ambapo takwimu hizo zionyesha kupungua kwa kipindi cha mwezi aprili hadi juni 2024 na kufikia vifo 9 vinavyotokana na changamoto hiyo.
Bi.Temu amesema kupungua kwa vifo hivyo kumetokana na mikakati mbalimbali waliojiwekea Idara ya Afya katika Halmashauri ya Arusha ikiwemo utoaji wa elimu kuhusu uzazi salama,mjamzito kuhudhuria kliniki kwa wakati pamoja na elimu juu ya lishe bora kwa mama mjamzito na watoto wachanga.
Ajenda Kuu za Kikao hicho ni pamoja na mkakatiti kambambe wa kuhakikisha Halmashauri ya Arusha endelea kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na watoto wachanga,kwa kuhakikisha elimu ya uzazi na lishe bora inaendelea kutolewa kwa mama mjamzito na watoto katika jamii pamoja na kuwasisitiza umuhimu wa kuhudhuria kliniki
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.