Na Elinipa Lupembe
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi zahanati ya Ilkirevi kata ya Olturo.
Mradi huo wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi umetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 50 fedha kutoka Serikali kuu, kwa lengo la kuboresha mazingira rafiki kwa wahudumu wa afya nchini.
Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, mhe. Dkt. ojung'u Salekwa licha ya kuridhishwa na utekezwaaji wa mradi huo, amewapongeza watalam wa halmashauri kwa usimamizi wa mradi huo na kuwataka kufanyia ushauri uliotolewa na madiwani pamoja na kurekebisha mapungufu yaliyoonekana.
Hata hiyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilkirevi, Mhe. Abraham Mollel, ameishukuru serikali kwa niaba ya wanachi wa kijiji hicho kwa kupeleka mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi kwenye zahanati yao.
"Tunaishukuru sana serikali kwa kutuletea mradi huu, kwa sasa daktari atahudumia wananchi muda wote tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo daktari, alikuwa anaishi mbali na kituo cha kazi na kupelekea wananchi kukosa huduma katika maeneo ya karibu, kwa sasa huduma zimeboreka". Ameweka wazi Mwenyekiti Mollel
Awali katika ziara hiyo, jumla ya Miradi 6 yenye thamani ya shilingi milioni 234.4, ikiwemo ujenzi wa nyumba ya mtumishi zahanati ya Ilkirevi, umaliziaji wa vyumba vitano vya madarasa na ofisi ya walimu, ukarabati wa kituo cha walimu - TRC Mringa, Kikundi cha vijana - KIDALI YOUTH GROUP, Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Lemugur, ujenzi wa uzio shule ya uzio wa shule ya msingi iliburu imetembelewa.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.