Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Arumeru, imefanya ziara ya kutembelea miradi mnne ya maendeleo, katika kata nne za halmashauri ya Arusha ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
Zaiara hiyo ya siku moja yenye lengo kukagua Miradi ya Maendeleo, inayotekelezwa katika ngazi ya halmashauri, imefanikiwa kupitia miradi iliyojikita kwenye sekta ya Elimu, Afya na miundombinu ya barabara miradi yenye thamani ya shilingi milioni 729.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Jerry Muro, ameitaja miradi hiyo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Losikito kata ya mwandeti, mradi uliohusisha ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, vyoo vya walimu na wanafunzi, nyumba ya walimu yenye sehemu za kuishi walimu watatu '3 in 1', na ukarabati wa jengo la utawala, mradi wenye thamani ya takribani milion 260 ikiwa ni pamoja na gharama za eneo hilo, fedha ambazo zimechangwa na wananchi kwa zaidi y asilimia 90%.
Miradi mingine ni ujenzi wa Kivuko cha Matevesi kinachounganisha wananchi wa kitongoji cha Ematasia na Ngorbob kivuko ambacho, kihistoria kilianza kwa msaada wa vifaa uliotolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, mradi ambao mpaka uategeea kukamilika hivi karibuni na unakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 25.
Aidha mkuu huyo wa wilaya ameendelea kufafanua kuwa, mradi mwingine ni mradi wa ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya Kituo cha Afya Mbuyuni uliogharimu, mradi unaohusisha ujenzi wa jengo la upasuaji, jengo la mama na mtoto, maabara na nyumba ya mtumishi, mradi wenye thamani ya shilingi milioni 400 fedha zilizotolewa na serikali kwa lengo la kuboresha huduma za afya.
Mradi mwingine ni ujenzi wa vyoo vya shule ya msingi Selian kata ya Kimnyaki, baada ya kutokea maafa ya, kutitia kwa choo kilichokuwa kinatumiwa na wanafunzi shuleni hapo, mapema mwezi uliopita.
Amesema kuwa, jumla ya vyoo viwili vyenye matundu kumi kila kimoja vinavyokadiriwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 22 kwa kila choo, na kufanya vyoo vyote kugharimu shilingi milioni 44, ikiwa ni fedha zilizotokana na michango ya wafadhili na wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na halmashauri ya Arusha kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, mheshimiwa Simon Ole Saning'o, licha ya kuipongeza ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru kwa usimamizi imara wa utekeleza wa Ilani ya CCM, amewapongeza pia atalamu wa halmashauri ya Arusha , serikali za vijiji, kata na wananchi wa maeneo yote yeye halmashauri ya Arusha na kuthibitisha kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, kutokana na miradi yote kutekelezwa kwa viwango.
Ameongeza kuwa, utekelezaji wa miradi hiyo unakwenda vizuri, ikiwa na ushiriki wa wananchi wa hali na mali katika maeneo husika, pamoja na kutekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaoridhisha huku akiwapongeza wananchi kwa kujitoa kushiriki, kuchangia miradi yote iliyopitiwa.
"Tunapita kukagua miradi ya maendeleo, ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, tunaridhishwa namna wananchi wanashiriki, hii inadhihirisha wananchi wanaielewa na kuiunga mkono Serikali ya CCM inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, endeleeni kuiamini serikali yenu" amesema Mwenyekiti huyo wa CCM.
Hata hivyo, wananchi wa maeneo hayo, wamepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano, kwa kupeleka fedha za miradi katika maeneo yao, pamoja na usimaizi unaoshirikisha wananchi moja kwa moja, ushirikishwaji unaosababisha miradi hiyo kwenda kwa kasi ikiwa na ubora tofauti na hapo awali ambapo ushirikishwaji wa wananchi kwenye miradi ulikuwa wa hali ya chini mno.
PICHA ZIARA.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, mhe. Jerry Muro akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM kukagua jengo la mama na mùtoto, kituo cha afya Mbuyuni , kata ya Oljoro.
Wajumbe wa kamati ya Siasa CCM- Arumeru, wakikagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, shule mpya ya Sekondari Losikito kata ya Mwandet.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM Arumeru, wakiwa kwenye mradi wa ujenzi wa vyoo, shule ya Msingi Selian ,kata ya Kimnyaki.
Jengo la shule mpya ya sekondari Losikito lenye vyumba vinne vya madarasa, moja ya mradi uliotembelewa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM Arumeru
Nyumba ya walimu yenye ehemu ya kuishi familia tatu ' in 1' , kwenye shule mpya ya sekondari Losikito, ikiwa ni moja ya mradi uliotembelewa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM Arumeru
Jengo la choo cha wanafunzi, shule mpya ya sekondari Losikito ni moja ya mradi uliotembelewa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM Arumeru
Jengo la maabara, kituo cha Afya Mbuyuni kata ya Oljoro, moja ya miradi iliyotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Arumeru.
Nyumba ya mtumishi, kituo cha Afya Mbuyuni kata ya Oljoro, moja ya miradi iliyotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Arumeru.
Jengo la mama na mtoto, kituo cha Afya Mbuyuni kata ya Oljoro, moja ya miradi iliyotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Arumeru.
Jengo la Upasuaji 'Theatre' kituo cha Afya Mbuyuni kata ya Oljoro, moja ya miradi iliyotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Arumeru.
Moja ya Jengo la choo vha matundu kumi, shule ya Msingi Seliani kata ya Kimnyaki, miongoni mwa miradi iliyotembelewa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Arumeru.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.