Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi anawakaribisha watumishi wote waliopangiwa na serikali kufanya kazi katika halmashauri ya Arusha.
"Jumla ya watumishi 65 wa sekta za elimu na afya, wamepangiwa kufanya kazi katika halmashauri yetu, walimu 6 wa shule za Msingi, walimu 34 kwa shule za Sekondari huku watumishi 28 wa kada tofauti wakipangiwa kufanya kazi katika Idara ya Afya". Amefafanua Mkurugenzi Msumi
Aidha amewapongeza watumishi hao kwa kupata nafasi hizo za kuwahudumia wananchi wa halmashauri ya Arusha.
"Maadili yetu ya Msingi, ni kufanya kazi kama timu"
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.