Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, anawatangazia wananchi wote, kutembelea Banda la Halmashauri yake katika viwanja vya maonesho Nanenane -Themi Jijini Arusha na kujionea shughuli za Kilimo na Ufugaji kwa vitendo.
Maonesho hayo yatakupa fursa zifuatazo:-
- Kujionea Teknolojia mbalimbali za Kilimo na Mifugo kwa ajili ya kufanya Kilimo Biashara na kukuza kipato na Uchumi wa nchi.
- Kutumia eneo dogo kwa kilimo cha mbogamboga kwa matumizi ya nyumbani.
- Kujifunza mnyororo wa thamani kwa kuchakata mazao ya Kilimo na Mifugo na kuyaongezea Thamani. Mfano mazao ya ngozi, nyama na maziwa.
- Kutumia kinyesi cha ng'ombe na kupata gesi 'Bio Gas'
"Karibuni nyote"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.