Na Elinipa Lupembe
Halmahauri ya Arusha imeadhimisha Juma la Elimu 2023 kwa kutoa tuzo kwa walimu na wadau wa elimu wanaochangia kukuza taaluma na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa shule za msingi na sekondari.
Jumla ya walimu 40 wamekabidhiwa vyeti na nishani kwa weledi wao katika kufundisha na kuwezesha ufaulu mkubwa wa wanafunzi kwa masomo wanayofundisha huku
wadau wa elimu, kutoka mashirika 14 wakipewa zawadi za uchangiaji sekta ya elimu katika halmashauri hiyo.
Akikabidhi zawadi hizo, Mgeni rasmi na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, licha ya kuwapongeza wanafunzi, walimu, wazazi na wadau wote wa elimu kwa kuwezesha halmashauri hiyo kufanya vizuri kitaaluma hususani kwenye mitihani ya wilaya, mkoa na Taifa, amewataka kuendelea kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora kwenye mazingira wezeshi.
"Serikali inatambua na kuthamini kazi kuwa inayofanywa na walimu ya kuondoa ujinga kwa wanafunzi licha ya changamoto nyingi zinazowakabili walimu, lakini juhudi zenu katika kukuza taaluma, zinathibitisha uzalendo mlio nao kwa nchi yenu, endeleeni kusimamia nidhamu na madili pamoja na usalama wa watoto wetu wawapo shuleni, niyashukuru mashirika yote na niwatake tuendelee kufanyakazi kwa weledi na kufikia malengo ya serikali" Amefafanua mkuu huyo wa wilaya.
Hata hiyo kaimu Afisa Elimu Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, ameweka wazi kuwa, wilaya Arumeru kupitia halmashauri zake mbili za Arusha na Meru, ndio zinaubeba mkoa huo kwa kufanya vizuri kwenye sekta ya elimu ikiwemo kitaaluma, utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo, utunzaji wa mazingira pamoja michezo kwa shule za msingi na sekondari.
"Ukiangalia shule zinazofanya vizuri kwenye mitihani ya mkoa na Taifa ziko Arumeru, mkoa unajivunia usimamizi imara wa fedha za serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo lakini zaidi kwenye suala zima la michezo ambapo mkoa unabebwa na wilaya hii ya Arumeru" Amebainisha Afisa huyo
Hata hivyo walimu na wadau wa elimu, wameishukuru na kuipongeza ofisi ya mkuu wa wilaya kupitia halmashauri ya Arusha kwa tuzo hizo zinazothibitisha kuthaminiwa kwa kazi kubwa inayofanywa na wadau wa elimu hudusani walimu wanaopambana na wanafunzi na kuhakikisha taifa linakuwa na wasomi wenye kutumia mbinu, stadi na maarifa katika kutumikia taifa kwenye sekta mbalimbali.
Mwalimu wa kujitolea shule ya sekondari Oldonyosambu, Mwl. Mathayo Meigaru, aliyepata zawadi ya kufanya vizuri katika kufundisha somo la Hisabati, amesema kuwa zawadi hizo ni motisha kubwa kwa walimu, inayowapa ari kuwaongezea juhudi na maarifa katika kazi, na kuahidi kuendeleza kuipigania nchi yake kupitia taaluma yake ya ualimu.
Naye Mratibu wa miradi, shirika la ACE Africa, Lukuba Mbozi, licha ya kuishukuru serikali kwa kutambua na kuthamini mchango wa wadau, amethibitisha kuwa zawadi hizo ni chachu ya maendeleo ya kusukuma zaidi gurudumu hilo, ili kufika malengo ya serikali ya kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bila kujali hali zao za kimaisha.
Halmashauri ya Arusha, imeathimidha Juma la Elimu 2023, kwa kutoa tuzo kwa walimu na wadau wa elimu katika halmashauri hiyo.
*ARUSHA DC Ni Yetu,Tushirikiane Kuijenga"
#KaziIendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.