Watalamu wa halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na wataalamu Washauri wa Don Consult Ltd wamefanya Mkutano na viongozi wa serikali, wazee wa mila na koo, watu mashuhuri na wawakilishi wa wananchi wa kijiji cha OLKOKOLA kata ya LEMANYATA kwa lengo la kuutambulisha mradi wa maji ambao uko katika hatua za awali za utekelezaji utakatekelezwa kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2017 mpaka Mei 2018.
Watalamu wameutambulisha mradi huo wa maji pamoja na kuielezea jamii umuhimu wa maji katika jamii, utunzaji wa mazingira ya vyanzo vya maji, usafi wa mazingira na usafi.Mradi huo wa maji unaenda sambamba na uchangiaji wa gharama za matumizi ya maji hayo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa kulipia maji kabla ya kutumia 'eWater paid' ili wananchi wafahamu uchangiaji wa huduma adi huu wa maji .
Mradi huo pia utaenda sambamba na utunzaji wa mazingira na ujenzi wa vyoo vya mfano katika maeneo ya tasisi na huduma za jamii kwa le go la kuifanya jamii kujenga vyoo bora katika kaya zao.
Wataalamu wa mazingira wamesisitiza utunzaji wa mazingira hasa ya vyanzo vya maji, maeneo itakayopita miundo mbinu ya maji pamoja na mazingira ya kuchotea maji.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.