Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Kenani Laban Kihongosi akikagua ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto Kituo cha Afya Oldonyosambu kata ya Oldonyosambu, ujenzi unaogharimu shilingi milioni 279 fedha kutoka Serikali Kuu kw aawamu mbili, ujenzi unaotegemea kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti,2025.
Kukamilika kwa jengo hilo kunaenda kukamilisha mkakati wa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Jemadari Dkt.Samia Suluhu Hassan la kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wakati wa kujifungua.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.