KITUO CHA AFYA NDURUMA CHAKABIDHIWA GARI LA WAGONJWA .
Kituo cha Afya Nduluma kilichopo Kata ya Nduruma katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kimekabidhiwa gari jipya la wagonjwa .
Gari Hilo limekabidhiwa ramsi na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe. Noah Lembris Saputu ikiwa ni sehemu ya juhudu za Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za Afya kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mhe.Noah amesema gari hilo litarahisisha usafirishwaji wa wagonjwa wa dharura na rufaa hususan kina mama kutoka Kituo cha Afya Nduruma kwenda Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Oltrumet au Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mt.Meru sambamba na kutoa huduma nyinginezo za Afya kwa wananchi.
" Kwa kweli tunamshukuru Mhe.Rais Dkt.Samia! amefanya kazi kubwa ya kuendeleza miradi mingi ya Umeme,Maji,Elimu,Barabara, Reli na leo mmeona katika sekta ya Afya tumeletewa gari ya wagonjwa ili kuboredha utoaji huduma kwa wananchi wa Nduruma,tunasema asante saana Mhe.Rais wetu" alisema Mhe.Noah
Kwa upande wake ,Diwani wa Kata ya Nduruma,mhe.Raymond Mollel amemshukuru Rais Dkt.Samia kwa kutoa gari la wagongwa kwa Kituo cha Afya Nduruma kwani litakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kata anayoiongoza kutokana na changamoto za usafiri kwa wagonjwa wa dharura iliyokuwa ikiwakabili hususan kwa kina mama.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Bw.Omary Sembe amemshukuru mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua changamoto mbalimbali kwa wananchi hususan katika kuendelea kusongeza huduma za Afya kwa Wananchi.
Bw.Sembe amesema gari hiyo ya Wagonjwa iliyokabidhiwa katika Kituo cha Afya Nduluma kutoka Serikali Kuu itakuwa msaada mkubwa kwa Wananchi wa Kata za Nduruma, Mlangarini,Bwawani na baadhi ya Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Meru hususan kina mama ambao walikuwa wanakabiriwa na changamoto ya usafiri wa kutembea zaidi ya km 40 hasa wanapopatwa na dharura ya kupelekwa kujifungua kwenye hospitali kubwa ya rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mt.Meru.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.